BREAKING NEWS : RAIS PIERE NKURUNZINZA AFARIKI DUNIA

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza aaga dunia kwa mujibu wa Msemaji wa Serikali, balozi Willy Nyamitwe, Rais Nkurunziza amefariki kwa mshtuko wa moyo kinyume na uvumi unaoenezwa.

Serikali ya Burundi imetangaza siku saba za maombolezi, Nkurunziza alizaliwa December 18, 1963 mwansiasa wa Burundi ambaye amekuwa madarakani tangu 2005.

Alikuwa Mwenyekiti wa Chama Tawala cha CNDD-FDD hadi alipochaguliwa kama Rais wa Burundi.

May 20, 2020 Burundi ulifanyika Uchaguzi ambapo alipatikana mrithi wake wa Urais ambapo miezi kadhaa nyuma alisema hatogombea tena

Comments