UCHAGUZI MKUU BURUNDI ,UPINZANI WADAI WATOA TUHUMA


Mikutano ya kampeni za kisiasa nchini Burundi inayofanyika wakati wa virusi vya corona imekua ikikosolewa

Upinzani pia umekua ukifanya mikutano mikubwa, kama huu


Shughuli za kupiga kura zimeisha mwendo wa saa kumi huku maafisa wa polisi wakisema kwamba uchaguzi huo ulifanyika kwa amani licha ya upinzani kudai kufanyika kwa udanganyifu na kukamatwa kwa wachiunguzi wa uchaguzi.
Wagombea wakuu Evariste Ndayishimiye kutoka kwa chama tawala na Agathon Rwasa wa upinzani , waliomba utulivu huku akisubiri matokeo yanayotarajiwa tarehe 25 mwezi Mei.
Tofauti na uchaguzi uliokuwa ukifanyika miaka ya nyuma , wakati huu ni tume ya uchaguzi pekee ilio na uwezo wa kutangaza matokeo.
Bwana Rwasa aliambia waandishi kwamba upinzani unashutumu kukamatwa kiholela kwa zaidi ya wachunguzi kumi katika vituo vya kupiga kura na makosa mengine ya uchaguzi.
Chama chake cha National Freedom Council CNL kimewalaumu wanachama wa chama tawala cha CNDD-FDD kwa udanganyifu unaoshirikisha , kupiga kura zaidi ya mara moja, kupiga kura kwa watu waliofariki pamoja na wakimbizi.
Tume ya uchaguzi au chama tawala hawajatoa tamko lao kuhusiana na madai hayo.
BBC imethibitisha kuwa mitandao ya Twitter, Whatsapp na Facebook kuwa haipatikani nchini humo.
Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa toka saa 12 asubuhi na vitafungwa saa 10 alasiri.
Wagombea saba wanawania hii leo kumrithi Pierre Nkurunziza, hata hivyo wagombea wawili ndio wanaopigiwa upatu zaidi, kutoka chama cha upinzani CNL Agathon Rwasa na chama tawala CNDD-FDD Evariste Ndayishimiye.
Raia wa Burundi wanapiga kura ya kumchagua rais, na katika karatasi za kupigia kura, jina la Pierre Nkurunziza halipo.
Siku ya leo inakamilisha utawala wa bwana Nkurunziza ambaye aliingia madarakani katika taifa hilo la Afrika Mashariki miaka 15 iliyopita.
Uchaguzi huo pia unahusisha nafasi za ubunge na madiwani. Matokeo yanatarajiwa kuanzia Mei 25
#chanzo BBC

Comments