Swali la mwandishi wa habari lamchefua Trump akatisha mkutano "Swali la kipuuzi kama hilo waulize China"

Rais Trump amelazimika kukatisha mkutano wake na waandishi wa habari baada ya kile kinachonekana ni kukerwa na swali la Mwandishi wa CBS Weijia Jiang ambaye alihoji ni kwanini amekuwa kama anashindana kila siku kwa kujigamba kuwa Marekani inaongoza kwa kupima corona kuliko Nchi zote Duniani, wakati Watu wanazidi kufariki nchini humo (zaidi ya vifo Elfu 81).

"Watu wanakufa kwa corona kila sehemu Duniani, sio Marekani tu, Swali la kipuuzi kama hilo waulize China sio mimi"- TRUMP

Comments