Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Stella Manyanya ameelekeza Viwanda ya plastiki nchini kuzalisha ndoo kwa wingi na ametoa onyo kali kwa wafanyabishara wanaouza bei za juu vifaa vya kunawia mikono.

Mhe. Stella Manyanya ametoa maagizo haya leo 02 mei 2020, Jijini Dar es salaam alipotembelea viwanda vinavyozalisha plastiki ambavyo ni kiwanda cha Silafrica Tanzania Ltd {Sumalia} na Kiwanda cha Cello Industries Ltd.

Aidha amevipongeza viwanda vyote kwa kuendele kuzalisha ndoo na vifaa vingine  kwa wingi vinavyotumika kunawia mikono ambavyo vinahitajika sana katika kipindi hiki cha mapambano dhidi ya ugojwa wa Corona.

“Nawapongeza na nimefurahishwa sana na uzalishaji mzuri na hakuna wasiwasi kwamba tutakuwa na upungufu wa ndoo za kunawia mikono katika maeneo yetu maana nimejionea uzalishaji mkubwa unaoendelea na ambao utaweza kukidhi maahitaji ya watanzania ya upatikanaji wa ndoo za kunawia mikono”

Aidha, ametoa onyo kali kwa wafanyabiashara wanaendelea kuuza bei Kubwa ndoo na vifaa vingine vya kunawia mokono kwa kufanya mapambano ya ugojwa huu kuwa fursa kwao ya kujinufaisha maradufu na kujipatia kipato kikubwa tofauti na ilivyokuwa awali.

“Natoa onyo kwa wafanyabiashara wote hasa wa reja reja kuna baadhi yao ambao wanatumia muda huu wa mapambano ya Corona kama fursa ya kujinufaisha maradufu, Ni marufuku kwa mtu yeyote kuongeza bei kupita kiasi maana kuna wafanyabishara wanaongeza mara mbili ya bei walizonunulia kiwandani”

Sambamba na hayo Mhe. Stella Manyanya ameendelea kusisitiza kuwa serikali itaendelea kufuatilia na kuwachukulia hatua wafanyabiashara wote wanaenda kinyume na maelekezo yanayotolewa na serikali kwa kuongeza bei bidhaa mbalimbali katika kipindi hiki cha Mfungo wa ramadhani pia cha mapambano ya Corona.

“Niendelee kuwakumbusha kuwa Serikali inaendelea kufanya msako mkali nchi nzima kwa wafanyabiashara wote wanaoenda kinyume na maelekezo ya serikali, kama tulivyofanya msako kwa wafanyabiashara wa sukari sasa tunaendelea kwa wafanyabiashara wanaouza vifaa vianavyotumiaka kunawia mikono

Comments