Mkurugenzi wa Upasuaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angella Muhozya akimuonesha Naibu Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile maendeleo ya afya ya mgonjwa aliyefanyiwa  upasuaji wa kupandikiza mshipa wa damu kwenye moyo (Coronary Artery Bypass Grafting-CABG). Mgonjwa huyo alifanyiwa upasuaji na wataalamu wa Taasisi hiyo ambapo Dkt. Ndugulile aliwatembelea wagonjwa waliofanyiwa upasuaji mkubwa wa kusimamisha moyo kwa ajili ya kuwajulia hali.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewataka wataalamu wa afya kuendelea kutibu watu wenye magonjwa mengine kama vile matatizo ya moyo na figo katika kipindi hiki cha ugonjwa wa Covid-19.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Faustine Ndugulile baada ya kuitembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na kuwaona wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa kupandikiza mishipa kwa wagonjwa wenye matatizo ya moyo.
Daktari bingwa wa wagonjwa walioko katika uangalizi maalum Said Kilindimo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  akimweleza Naibu Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile jinsi wanavyowahudumia wagonjwa walioko katika chumba hicho. Dkt Ndugulile alitembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kuwajulia hali wagonjwa waliofanyiwa upasuaji mkubwa wa kusimamisha moyo.

Naibu Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa chumba cha wagonjwa walioko katika uangalizi maalum (ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati alipotembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kuwajulia hali wagonjwa waliofanyiwa upasuaji mkubwa wa kusimamisha moyo.

Dkt. Ndugulile amesema pamoja na kuwapo kwa maambukizi ya ugonjwa wa Corona, watu wenye matatizo ya moyo, kupumua, figo, kisukari pamoja na matatizo mengine wanapaswa kupatiwa matibabu.

“Tunaweza tukawa tunapambana na Corona, tukawapoteza wagonjwa wengi kwa sababu tu hatujaweza kuwapatia huduma ya matibabu ya kisukari, figo, presha au moyo, hivyo nitoe rai kwa wahudumu wa afya wahakikishe wanaendelea kuwatibu watu wenye magonjwa haya pamoja na magonjwa mengine,” amesema Dkt. Ndugulile.
Naibu Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua taarifa za mgonjwa aliyefanyiwa  upasuaji wa kupandikiza mshipa wa damu kwenye moyo (Coronary artery bypass grafting (CABG) na wataalamu wa upasuaji wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Dkt Ndugulile alitembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kuwajulia hali wagonjwa waliofanyiwa upasuaji mkubwa wa kusimamisha moyo.

Katika hatua nyingine, Dkt. Ndugulile amewapongeza wataalamu wa JKCI kwa kufanya upasuaji wa kupandikiza mishipa kwenye moyo kwa wagonjwa waliokuwa na matatizo ya moyo. 

 “Sisi kama Wizara ya Afya, tunapata faraja sana, mambo kama haya ni mazuri na lazima tuseme kwa hiyo hii operesheni mliofanya ni kubwa na nje ya nchi ingetugharimu shilingi milioni 80 hadi 90 kwa mtu mmoja, lakini hapa tumefanya kwa shilingi milioni 29 kwa kutumia wataalamu wetu na wagonjwa wetu wanaendelea vizuri,” amesema Dkt. Ndugulile. 
Naibu Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akimjulia hali mgonjwa aliyefanyiwa  upasuaji wa kupandikiza mshipa wa damu kwenye moyo (Coronary Artery Bypass Grafting-CABG) na wataalamu wa upasuaji wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Dkt Ndugulile alitembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kuwajulia hali wagonjwa waliofanyiwa upasuaji mkubwa wa kusimamisha moyo.
Amesema awali wataalamu kutoka nje ya nchi walikuwa wanakuja kufanya upasuaji kama huo, lakini sasa Watanzania wazalendo wanafanya baada ya kutoa mishipa kwenye paja na kwenye kifua cha mgonjwa husika.

“Leo nimekuja kuona kazi kubwa iliyofanywa na wataalamu wazalendo wa JKCI ya upasuaji wa kupandikiza mishipa kwenye moyo ili uweze kufanya kazi kwa wagonjwa waliokuwa wakikabiliwa na matatizo ya moyo,” amesema Dkt. Ndugulile.

Naibu Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa chumba cha wagonjwa walioko katika uangalizi maalum (ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati alipotembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kuwajulia hali wagonjwa waliofanyiwa upasuaji mkubwa wa kusimamisha moyo. Kushoto  ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi. Picha na Jackson Monela - WAMJW

Na John Stephen, WAMJW – Dar es Salaam






Naye Mkurugenzi wa Upasuaji wa JKCI, Dkt. Angella Muhozya amesema kuwa wagonjwa wote waliofanyiwa upasuaji na wataalamu wazalendo wanaendelea vizuri na kwamba wataruhusiwa muda wowote kuanzia sasa.

Mmoja wa wagonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa moyo, Bw. Hamid Nassoro amesema baada ya kufanyiwa upasuaji hivi sasa anaweza kuzungumza vizuri tofauti na awali alikuwa hawezi kuzungumza na kwamba tayari ameshaanza mazoezi.

Comments

  1. Making Money - Work/Tennis: The Ultimate Guide
    The goyangfc.com way you would expect from betting on the tennis matches งานออนไลน์ of tennis is septcasino.com to bet on the player you like https://sol.edu.kg/ most. But you also need a gri-go.com different

    ReplyDelete

Post a Comment