MBUNGE AUNGANA NA WANANCHI KUPAMBANA NA CORONA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana Ccm Wilaya ya Bukombe Nelvin Salabaga Ndugu  aliwataka Maafisa Watendaji kugawa vifaa vya kunawia kwa wananchi hasa kwenye maeneo yenye msongamano wa watu wengi ili kufikia malengo ya Mbunge Biteko ya kuungana na wananchi na serikali kujikinga na ugonjwa wa COVID 19 ambao bado ni janga la kidunia.

 Wito huo ulitolewa na Mwenyekiti huyo wakati akikabidhi vifaa toka kwa Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko ambavyo ni  ndoo 100 na mabeseni 100 kwa watendaji wa kata.

“Nampongeza Mhe Biteko kwa hatua hiyo ya kuwajali wananchi wa Bukombe katika mapambano dhidi ya Corona”Alisema Ndugu.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Vijana alitoa wito kwa wadau mbalimbali kumuunga mkono Mbunge Biteko kwa jitihada alizozionyesha

Kwa upande wake Afisa mtendaji kata ya Katente Issa Mushule  alisema kupitia msaada huo wananchi wataendelea kupata hamasa ya kujikinga.

Comments