Home BREAKING NEWS BREAKING NEWSHabarikitaifa BREAKING NEWS: Wabunge wawili wahama CHADEMA




WABUNGE wa Viti Maalum CHADEMA, Joyce Sokombi na Susan Masele wakizungumza na wanahabari leo.
Na Joyce Kasiki, Dodoma
WABUNGE wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Joyce Sokombi na Susan Masele wametangaza kuhamia Chama cha NCCR-Mageuzi mara baada ya Bunge kumaliza muda wake, Juni 19, mwaka huu.
Wabunge hao wametangaza uamuzi huo leo jijini Dodoma wakati wakizungumza na waandishi wa habari. Wametaja sababu za kufikia uamuzi huo ni pamoja na madai ya Katiba ya CHADEMA kuvunjwa na baadhi ya wanachama kufukuzwa uanachama bila kupewa nafasi ya kusikilizwa.
“Kuna unyanysaji dhidi ya wanawake na madaraka kuhodhiwa na wanaume, hivyo kusababisha unyanyasaji kijinsia wa kingono,” alidai Susan na kuongeza kwamba ndani ya chama hicho kuna makundi ya kibaguzi hadi bunguni huku wengine wakionekana ni wapiga makofi bungeni na wengine ndio wakiwa wachangiaji bungeni.
Hivi karibuni wabunge wawili wa CHADEMA walitangaza kuhamia NCCR-Mageuzi mara baada ya Bunge kumaliza muda wake, Wabunge hao ni Joseph Selasini (Rombo) na Anthony Komu (Moshi Vijini)

Comments