CORONA:MAREKANI YARIDHIA DAWA HII KUTUMIKA

Mamlaka ya dawa na chakula nchini Marekani (FDA) imetoa ruhusa ya dharura ya dawa ya Ebola inayofahamika kama 'remdesivir' kutumika kuwatibia wagonjwa wenye virusi vya corona.
Ruhusa ya kutumika kwa dawa hiyo kwa sasa imetolewa kwa watu ambao wamelazwa hospitalini tu kutokana na ugonjwa wa Covid-19.
Jaribio la hivi karibuni la kitabibu linaonyesha kuwa dawa hiyo inaweza kuwasaidia watu mahututi wanaoumwa corona, na inaaminiwa kuwa inaweza kuwasaidia kupona haraka.
Hatahivyo, haijaonyesha kuwa inasaidia kupunguza idadi ya vifo.
Wataalamu wa dawa wametoa onyo kuhusu dawa hizo -ambazo zilitengenezwa ili kutibu Ebola, na zilitengenezwa na kampuni ya Gilead pharmaceutical iliyopo mjini California -kwamba visionekane kuwa ni jambo la ajabu sana kwa dawa hiyo kuanza kutumika kwa ajili ya kutibu virusi vya corona.
Dawa hiyo inaweza kuigwa na kuharibu utendaji wake.
Katika kikao na rais wa Marekani Donald Trump katika ofisi za Oval, Mkurugenzi mkuu wa Gilead Daniel O'Day alisema Mamlaka ya dawa FDA ndio hatua muhimu ya kwanza.
Kampuni hiyo itachangia chupa za dawa hiyo milioni 1.5 , alisema.
Kamishina wa FDA, bwana Stephen Hahn alisema kwenye mkutano huo: "Hii itakuwa tiba ya kwanza ya Covid-19 kupitishwa , tumefurahi sana kuwa sehemu ya uwezeshaji huo."
Mamlaka ya dharura ya FDA si sawa na ile ambayo inatoa idhini rasmi ambayo inahitaji uangalizai wa hali ya juu zaidi.
Chati ya njia za kujikinga corona

NI NINI TUNAFAHAMU KUHUSU REMDESIVIR?

Dawa hii haikutibu Ebola, na Gilead ilisema kwenye mtandao wake: "Remdesivir ni dawa ya majaribio ambayo haina ufanisi au usalama wa kutibu magonjwa yote." Gilead ilitoa angalizo la madhara makubwa ambayo yanaweza kumpata.
Ingawa rais Trump amekuwa akiiunga mkono remdesivir kwa kuizungumzia kuwa ni dawa sahihi ya virusi vya corona.
Katika jaribio la kitabibu, taasisi ya taifa ya mzio na magonjwa yanayoambukiza nchini Marekani (NIAID) imebaini kuwa remdesivir inapunguza muda wa dalili za ugonjwa huo kutoka siku 15 mpaka siku11.
Jaribio la dawa hilo lilifanyika kwa watu 1,063 katika hospitali mbalimbali duniani, - zikiwemo Marekani, Ufaransa, Italia,Uingereza, China na Korea kusini. Baadhi ya wagonjwa walipewa dawa hiyo na wengine walipewa tiba ya 'placebo'.
Dkt Anthony Fauci ambaye anaiongoza NIAID,alisema kuwa remdesivir imeonyesha wazi umuhimu wake ,kikubwa ni kuharakisha muda wa mtu kupona.
Hata hivyo remdesivir inaweza kusaidia katika uponyaji - na kuzuia watu kutibiwa kwenye chumba cha dharura - majaribio ya dawa hiyo haijaonyesha wazi kuwa inaweza kuzuia watu kufa kutokana na virusi vya corona.
Maswali mengi yakiwa hayana majibu bado kuhusu muongozo wa tiba hiyo , Gilead alishauri kuwa wagonjwa watumie dozi ya siku kwa wale ambao wanatumia mashine ya kupumulia na siku tano kwa wagonjwa ambao hawatumii mashine.

JE, MATAIFA MENGINE YANAWEZA KUTUMIA DAWA HIYO YA REMDESIVIR?

Gilead alisema kwa sasa wanatumia dawa ambazo zilikuwepo kwenye hifadhi ya dawa zao na si rahisi kusafirisha maeneo mengine.
Serikali ya Marekani itaweza kupanga namna remdesivir itafikishwa kwenye hospitali za kwenye miji mbalimbali nchini Marekani , ambayo imeathirika zaidi na ugonjwa huu wa Covid-19.
Hivyo haiko wazi kabisa , ni kiasi gani cha dawa kitasambazwa duniani kote na hata gharama yake haijajulikana bado.
Gilead imesema kuwa inachangia dozi milioni 1.5 ya dawa hiyo ya remdesivir, ambazo zitakuwa na uwezo wa kutibu watu zaidi ya 140,000 bila gharama yoyote ile.Kitengo cha dharura cha kusambaza dawa nchini Marekani kinahusika katika hilo

#chanzo chetu BBC

Comments