UVCCM YA TOA PONGEZI KWA WADAU WA MAENDELEO



Umoja wa Vijana UVCCM Wilaya ya Bukombe Mkoa wa Geita umewapongeza wadau wa maendeleo Wilayani hapa kwa kuchangia ujenzi nyumba ya Katibu wa jumuiya hiyo.

Kauli hiyo ilitolewa na mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Bukombe Nelvin Salabaga wakati alipokuwa ametembelea ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Jumuiya Umoja wa Vijana .

Salabaga alisema ujenzi huo ulianzishwa na jumuiya hiyo Februari 17 mwaka huu na wanatarajia kukamilisha Mei 2020  kwa kutumia nguvu za wadau na michango ya vijana.

Katibu wa Jumuiya ya Vijana UVCCM Wilaya ya Bukombe Philbert Ngemela alisema ujenzi utakapo kamilika utamuondolea changamoto ya kutembea umbali mrefu anapo kuwa anaenda kutekeleza majukumu yake.

Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi na Afisa Tawala Wilaya AlLy Mketo alisema wamepokea michango mbali mbali toka kwa wadau zikiwemo tofari 2000 zenye thamani ya Tsh milioni 2 toka kwa Mbunge Jimbo la Bukombe Mhe, Doto Biteko.

Mketo alitoa wito kwa wadau wa maendeleo kuendelea kuchagia ili kufanikisha ukamilishaji wa ujenzi huo.

Comments