SERIKALI YA TUMIA TSH MILIONIN 146.6 KUWAKWAMUA WANAWAKE KIUCHUMI


 

Serikali kupitia mapato ya ndani ya  Halmashauri ya Wilaya Bukombe mkoani Geita imetoa mkopo wenye mashariti nafuu  kwa lengo la kuwa kwamua kiuchumi  kuanzia ngazi ya familia.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba kwenye sherehe ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani iliyofanyika kiwilaya katika uwanja wa Mwenge kata ya Uyovu.

Nkumba alisema serikali itahakikisha inaendea kuimarisha kundi la wanawake katika frusa za maendeleo ikiwa Tsh milioni 146.6 zimekopeshwa kwa mashariti nafuu kwa wanawake 575 vikundi 75.

 Alisema mwaka 2018/19 vikundi 35 wanawake 175 walikopeshwa Tsh milioni 62.2 na 2019/20 vikundi 40 ambavyo vinawanufaika wanawake 400 walipewa Tsh milioni 84.6.

 Miongoni mwa wanufaika wa mikopo ya serikali Conjester Mwita alisema tangu aanze ujasiliamali kupitia mikopo inayo tolewa na serikali kwa mashariti nafuu amefanya maendeleo kwa kukuza kipato cha familia na kuinuka kiuchumi.

Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Bukombe Mariana Genya alisema Januari mwaka huu hadi Machi vikundi 13 vinatarajia kupewa mkopo wa Tsh milioni 38.5 vimesha tembelewa na kukizi vigezo.

Wakati huo huo wanawake walishiriki shughuli za ujenzi vyumba vya madarasa shule ya Sekondari Uyovu kwa kusomba mawe  kwa mjibu wa Mkuu wa Shule hiyo Simon Mashauri alisema mahitaji ya madarasa 24 yaliyopo 9 upungufu 15 ingawa kunahatua mbali mbali za ujenzi vyumba vinne vya madarasa kwa nguvu za wananchi na Mkuu wa Wilaya

Akitoa shukran kwa niaba ya wanawake wa Bukombe Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake wa Mkoa wa Geita Jazaa Komba alianza kwa kutoa shukrani za dhati kwa Mbunge wa Jimbo la   Bukombe   Doto Mashaka    Biteko kwa jinsi anavyo washika mkono wamama wajasiriamali.

“Mhe  Biteko mbali na kututafutia fedha serikalini bado anatoa fedha zake za mfukoni  ili sisi wamama wa Bukombe tuinuke kiuchumi”.Alisema Komba  


Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wila ya Bukombe Dionis Myinga kwa pamja wakishiriki
shughuli za ujenzi vyumba vya madarasa shule ya Sekondari Uyovu kwa kusomba mawe kwenye siku ya wanawake Duniani









Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba akiwa na baadhi ya wamama wakishiriki katika zoezi la upandaji miti Shule ya sekondari Uyovu.
 
Wamama wakishiriki katika zoezi la upandaji miti Shule ya sekondari Uyovu.


Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba akisoma lebo ya bidhaa iliandaliwa na Bafremi Enterprises ambao wanahusika na utengenezaji na uuzaji wa sabuni aina mbalimbali za kunawia mikono,kufulia,kudekia na kuondoa harara na epele pamoja na ushonaji wa masweta na mazuria


Mama Angel Decoration ambae ni mtengenezaji wa keki na mapambo akimuonyesha Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba namna ya utengeneji wa vitu hivyo


Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wila ya Bukombe Dionis Myinga wakiwa viongozi mbalimbali wa chama na serikali wakiwa kwenye banda la mama mjasiriamali anaejihusisha na utengenezaji wa Chaki(Bukombe Chalk)


Diwani wa Kata ya Bukombe Mhe Rozalia Msokola akizungumza kwenye sherehe ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani iliyofanyika kiwilaya katika uwanja wa Mwenge kata ya Uyovu.

Diwani Viti maalum Tarafa ya Siloka Mhe Elizabeth Ngasa akizungumza kwenye sherehe ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani iliyofanyika kiwilaya katika uwanja wa Mwenge kata ya Uyovu.

Comments