RADI YAUWA NG’OMBE 26


 Radi yauwa ng’ombe 26 Kitongoji cha Sigoba Kata ya Runzewe Mashariki Wilaya ya Bukombe Mkoa wa Geita, wamekufa kwa kupigwa radi wakati wakipata malisho hapo kijijini.

Afisa Mtedaji wa Kijiji cha Msonga Andrew Tungu aliwataja wamiliki wa ng’ombe  zilizo pigwa radi na kufa papo hapo  Bundala  Saliboko  ng’ombe sita Joseph  Mhangwa ng’ombe sita Shikome Mlekwa ng’ombe sita Christopher Aloyce ng’ombe wanne  Cecilia Sengerema ng’ombe watatu Ndaki Paul ng’ombe mmoja wote wakazi wa kijiji cha Msonga. 

Nae Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba wakati akitoa pole kwa niaba ya serikali kwa wafugaji aliwataka kuwa wavumilivu na kuto ingiza imani za kishirikina kwani  radi hupiga vitu mbali mbali zikiwemo nyumba hata  binadamu. 

Nkumba alitoa wito kwa waganga wa tiba asilia kutokuwa nyuma ya hili kwa kupiga ramri choganishi kwa wafugaji na kusababisha uhasama kwa jamii .

 Kwa upande wao wafugaji Sengerema alisema ni mipango ya mungu radi kuuwa ng’ombe huku Mhangwa akiongeza kuwa hawawezi kuingiza imani za kishirikina ingawa kila mtu anamtazamo wake.

Comments