NAIBU KATIBU MKUU CCM TANZANIA BARA AWASHUKIA WANAOJIPITISHA KABLA YA MDA


 Naibu Katibu Mkuu wa Ccm Tanzania Bara Ndg Rodrick Mpogolo akiwahutubia
wenyeviti wa mashina(Mabalozi) wa Kata tatu za Wilaya ya Bukombe 


  Naibu Katibu Mkuu wa Ccm Tanzania Bara Ndg Rodrick Mpogolo akiwakabidhi vitambulisho mabalozi ili awaweze kutambulika

  Naibu Katibu Mkuu wa Ccm Tanzania Bara Ndg Rodrick Mpogolo akipokea zawadi ya asali kutoka kwa Mwenyekiti wa Ccm Wilaya ya Bukombe Daniel Mchongo kwa niaba ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Bukombe



Naibu Katibu Mkuu wa Ccm Tanzania Bara Ndg Rodrick Mpogolo amewashukia wanaojipitisha kwenye Kata na Majimbo wakiwania uwakilishi kabla ya mda wa uchaguzi kufika.

Aliyasema hayo wakati akizungumza na wenyeviti wa mashina(Mabalozi) wa Kata tatu za Wilaya ya Bukombe baada ya kikao  na wajumbe wa sekretarieti ya Ccm wa Wilaya zote na Mkoa wa Geita wakati wa ziara yake ya kwenda anaimarisha chama na jumuiya zake.

Aidha amewataka viongozi walioko madarakani kuanzia ngazi ya Matawi  kuwaheshim mabalozi  kwani wao ndio wenye watu na ndio mwanzo wa muundo wa muundo wa chama na serikali.

Mpogolo aliwapongeza sana wanachama wa Ccm kwa kushirikiana vyema na wananchi wa Bukombe kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa kumchagua Mhe Doto Mashaka Biteko kuwa Mbunge ambae sasa ni Waziri wa Madini.

“Mhe Biteko ni kiongozi shupavu mwenye uthubutu na mwadilifu anaefanya kazi kwa weledi katika majukumu yake kama Waziri mwenye Wizara nyeti akimsaidia Rais wetu mpendwa huku akizidi kuisukuma Bukombe iende kwa kasi katika maendeleo naomba tumuunge mkono” Alisema Mpogolo.

Nae Mwenyekiti wa Ccm Wilaya ya Bukombe Daniel Mchongo wakati akifunga kikao hicho alisema kupitia ziara ya kiongozi huyo wa kitaifa wamejifunza mengi na kumhakikishia kiongozi huyo kuyafanyia kazi maelekezo aliyoyatoa kwa wakati.

“Yeyote anaewania nafasi  ya uwakilishi kabla ya mda kwa Bukombe tutashughulika nae kwa mjibu wa kanuni za chama chetu” Alisisitiza Mwenyekiti Machongo.

Comments