DC AWAONYA WATUMISHI WANAOKWAMISHA MAENDELEO

 Mkuu wa wilaya ya Bukombe mkoani Geita, Said Nkumba akiwahutubia
wajumbe wa kamati za maendeleo tarafa ya Siloka inayoundwa na kata tano.

 Katibu tawala wa wilaya ya Bukombe Paul Cheyo akitambulisha safu aliyoambatana nayo


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bukombe Dioniz Myinga akizungumza na wajumbe wa kamati za maendeleo tarafa ya Siloka inayoundwa na kata tano.
 







Mkuu wa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, Said Nkumba amewaonya baadhi ya watumishi wa Serikali  wanaokwamisha miradi ya maendeleo kukamilika kwa wakati iliyoibuliwa na wananchi kwa muda mrefu. 

Nkumba aliyasema hayo kwenye kikao cha kazi kilichokuwa kimejumuisha wajumbe wa kamati za maendeleo tarafa ya Siloka inayoundwa na kata tano.

Nkumba alianza kwa kupongeza watumishi wanaofanya vizuri katika kusimamia miradi kisha kuwageukia ambao hawashiriki kikamirifu na kukwamisha miradi hiyo kukamirika.

"Mbunge wa jimbo la Bukombe Doto Biteko amekuwa akishirikiana na wananchi kwa kujitoa vifaa mbali mbali vya ujenzi  na fedha kwenye miradi lakini wapo watumishi ambao hawasimamii kikamilifu ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati na ikiwa katika ubora mzuri".Alisema Nkumba
 
Nkumba alitoa wito kwa wenyeviti wa vitongoji na vijiji kushirikina na maafisa watendaji wa vijiji na kata ili kuhakikisha miradi inakamilika na kuwashirikisha wananchi ili wanufaike na fedha ambazo zinaletwa na serikali walioiweka madarakani.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Bukombe Dioniz Myinga aliwasihi maafisa watendaji wa kata kugawa madarasa kwenye vitongoji ili wachange na kukamirisha ujenzi.

Myinga aliwaomba kusimamia michango ya wananchi kikamirifu na kuwa wawazi juu ya makusanyo ya fedha ambazo zimekusanywa ikiwemo  kuzingatia muda waliojiwekea.

Comments