Mbunge wa jimbo la Bukombe Doto Biteko akihutubia kwenye mkutano wa hadhara kijiji cha Bulama
Katibu wa itikadi na uenezi CCM wilaya ya Bukombe Ladislaus Soku akimpongeza Mhe. Biteko kwanamna anavyochangia maendeleo kwa wananchi
Muonekano wa jengo la shule ya msingi Bulama Baada ya nguvu za wananchi na wadau mali mbali wa elimu akiwemo Mbunge wa jimbo la bukombe Mhe. Doto Biteko
Wananchi wa kijiji cha Bulama kata ya Runzewe mashariki wilaya ya Bukombe mkoani Geita, wameanza kuchagishana sh 1500 kila mtu Mwenye uwezo wa kufanya kazi ili kukamilisha ujezi wa shule ya msingi Bulama.
Afisa mtendaji wa kijiji cha Bulama Andrew Mbikilwa alisema wananchi walianza kujichagisha sh 1500
kila mtu wenye uwezo wa kufanya kazi Novemba 2017 mradi utakamilika Desemba
2020.
Mbikilwa alisema mradi huo hadi kukamilika madarasa matatu na
ofisi moja itagharimu sh 12.7 milioni
wananchi wamesha changia sh 10.6 milioni wadau wa maendeleo wametoa sh
6000 na ujenzi uko hatua ya lenta kwa thamani ya sh 11.2 milioni.
Mbunge wa jimbo la Bukombe Doto Biteko akiwa kijiji
cha Bulama alipokwenda ziara kuhamasisha maendeleo aliwaunga mkono wananchi mifuko 160 ya
saruji na mabati pamoja na misumari
Biteko alitoa wito kwa viongozi wa serikali kuacha kutumia
nguvu nyingi kukusanya michango kwa wananchi ikiwa wengine wanajitolea nguvu
zao kwa kusogeza mchanga, mawe, maji wengine wanachagia mali zao.
Nae Mkazi wa kijiji cha Bulama Siphania Daniel alisema kupitia
mchango wa Mbunge Biteko amewahamasisha kuchagia ili mradi huo ukamilike ambao
utaondoa adha ya kutembea umbali mrefu kwenda Kufuata elimu.
Comments
Post a Comment