WANANCHI WA ASWA KUACHA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI

 
  Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba akihutubia wananchi na watumishi wa mahakama mkoa wa Geita siku ya maadhimisho ya wiki ya sheria. 


 Mkuu wa Mashtaka Mkoa wa Geita Bibiana Kileo akisoma taarifa ya utekelezaji wa sheria mahakamani.

 Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Geita Obadia F. Bwegoge akisema waliyoyafanya na changamoto.


Mawakili wa kujitegemea na mawakili wa serikali na watumishi wengine wa mahakama wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi.
 Wandesha Mashtaka wa Serikali na Mawakili wa kujitegemea wakiwa kwenye picha ya pamoja na Meza Kuu.

 Kamati ya Usalama Mkoa wa Geita na Viongozi mbalimbali wa Serkali wakiwa na mgeni rasmi katika picha ya pamoja baada ya maadhimisho ya wiki ya sheria kimkoa.


  Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba na
 Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Geita Obadia F. Bwegoge wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi waliohudhuria kwenye viwanja vya maadhimisho ya wiki ya sheria.


Wananchi Mkoani Geita wametakiwa kuachana na tabia ya kujichukulia sheria mkononi wanapowakamata waharifu bali washirikianane na vyombo vinavyosimamia sheria.

Rai hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Robert Gabriel katika maadhimisho ya Wiki ya sheria Ki mkoa yaliyofanyika katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya ya Geita.


Nkumba amesema kauli mbiu ya maadhimisho ya Wiki ya sheria 2020 ni "UWEKEZAJI NA BIASHARA: WAJIBU WA MAHAKAMA NA WADAU KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI YA UWEKEZAJI"  na ili kufikia malengo hayo wananchi wanapaswa kuwa wazalendo  kwa kuishi kwa kuheshimu sheria.


Kwa upande  Mkuu wa Mashtaka Mkoa wa Geita Bibiana Kileo alisema kupitia mabadiliko ya sheria ambayo yametoa nafasi ya kumaliza kesi za jinai kwa njia ya makubaliano ya kukiri
Kileo amesema kupitia mahakama ya hakimu mkazi wameendesha jumla ya kesi 13 ikiwa kesi 10 niza uhujumu uchumi na kuokoa fedha Tsh bilioni 2 kutoka kwa washtakiwa 101 ambao mpaka sasa wako huru.


Aidha Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Geita Obadia F. Bwegoge alisema kutokana na kutokua na Mahakama kwa baadhi ya Wilaya ikiwemo Mbogwe na Nyah'gwale  wananchi wanalazimika kufuata huduma hizo kwenye Wilaya jirani.


Bwegoge alisema kupitia changamoto hizo aliwahakikishia wananchi kuwa mwaka huu Mahakama zitaanza ndani ya Wilaya hizo katika majengo yatakayokuwa yametengwa na serikali kwa ajili ya Mahakama.

Comments