WAMAWAKE WAASWA KUPAMBANA NA MAAMBUKIZI YA UKIMWI


Wadau wa kupambana na maambikizi ya Ukimwi wakiwa kwenye warsha ya kudhibiti UKIMWI iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Biteko kwa kushirikiana na shirika la International Control Aids Program I.C.A.P.


Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Biteko akiwataka wanawake kuendelea kuelimisha jamii juu ya maambukuzi ya virusi vya ukimwi

Afisa Tawala wa Wilaya ya Bukombe Ally Mketo wakati akifungua warsha ya kudhibiti UKIMWI iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Biteko kwa kushirikiana na shirika la International Control Aids Program I.C.A.P.

Wanawake Wilayani Bukombe wakipewa  mafunzo ya kudhibiti UKIMWI



Wanawake Wilayani Bukombe Mkoa wa Geita wameaswa kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya maambukizi ya Ukimwi .

Aliyasema hayo Afisa Tawala wa Wilaya ya Bukombe Ally Mketo wakati akifungua warsha ya kudhibiti UKIMWI iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Biteko kwa kushirikiana na shirika la International Control Aids Program I.C.A.P.

“Takwimu za mwaka 2019 watu waliopima na kukutwa na maambukizi ni 2576 ikiwa wengi wao ni wanawake ambao ni  1678 na wanaume 897 hali ambayo ina pelekea kuwa hali ya maambukizi kufikia asilimia 5.3 wilayani hapa”.Alisema Mketo

Nae Mratibu wa Shirika I.C.A.P. Mkoa wa Geita Mwedi Mohamed alisema wametoa mafunzo ya kujikinga na UKIMWI kwa watu 250 Wilaya ya Bukombe ikiwa lengo la utowaji wa Elimu hiyo ni kuhakikisha ifikapo  mwaka 2030 asilimia 95 ya watanzania wawe wanajua hali zao, na asilimia 95 wawe wameuganishwa kwenye huduma ya dawa, huku asilimia 95 wawe wamefubaza UKIMWI.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Biteko  alimuomba Mkurugenzi Mkuu wa shirika la International Control Aids Program I.C.A.P linalo toa Elimu kwa makundi mbali mbali ili kuepuka na maambukizi ya UKIMWI Tanzania Dk Fernado Morales kuendelea kuwaelimisha wanawake kupima na kujikinga na maabukizi.


Comments