WAKULIMA 36207 WAPEWA ELIMU YA TEKNOLOJIA YA KILIMO


 Viongozi wa CCM ngazi ya Wilaya wakiwa  Meza Kuu 

 Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba akitoa taarifa ya utekelezaji wa serikali ilani ya uchaguzi wa CCM 2015 hadi 2020
 



Wajumbe wa kikao cha halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Bukombe mkoa wa Geita, wakipitia kabrasha la taarifa ya utekelezaji wa serikali ilani ya uchaguzi wa CCM 2015 hadi 2020 taarifa ambayo ilikuwa ina tolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba kuanzia mwezi Julai hadi Desemba 2019


Wakulima 36207 Wilaya ya Bukombe Mkoa wa Geita, wamepewa Elimu ya matumizi ya teknolojia ya kisasa na zana za kilimo ili kuweza kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba aliyasema hayo kwenye kikao cha  Halmashauri  Kuu ya CCM Wilaya wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya 2015 hadi 2020 kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2019.

Nkumba alisema serikali imetilia mkazo na kuimarisha upatikanaji wa pembejeo na zana za kilimo ili kuongeza uzalishaji kwa kuzingatia matumizi ya teknolojia ili kuinua uchumi wa mwananchi wa Wilaya ya Bukombe hadi taifa.

Nkumba alisema serikali kwa kutekeleza ilani ya CCM imeboresha mfumo wa utoaji wa ruzuku za pembejeo za kilimo ikiwa jumla ya wakulima 14,608 wilayani hapa wamepewa ruzuku za mbegu ya pamba tani 152,  tani za mbolea 782 tani 102 za mbegu bora za mazao ya chakula imenunuliwa kwenye maduka 41 ya pembejeo ya watu binafsi. 

Nkumba aliongeza kuwa Halmashauri imepokea dawa zenye thamani ya 147.8 milioni na kugawa madawa kwenye hospitali ya wilaya, vituo vya afya vinne na Zahanati tatu”

Nkumba alisema serikali imekuwa ikihamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya ya jamii (CHF) na Julai hadi Desemba 2019 wananchi 381 walikuwa wamejiunga. 

Pia Nkumba alisema halmashauri ya wilaya ya Bukombe imetumia sh 49.7 milioni kwa ajili ya kutowa huduma ya chanjo ya surua rubela kwa watoto 58,404 chini ya miaka mitano.

Alisema Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe  imekopesha sh 31.7 milioni kwa vijana wanawake na watu wenye ulemavu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukombe Daniel Machongo alisema wajumbe kwa tarifaa hiyo wamelizika kwa asilimia 100.

Machongo alielekeza serikali kufanya mambo yanayoihusu jamii moja kwa moja kama Afya yapewe kipaumbele  hasa kwa mwaka huu kuelekea kwenye uchaguzi mkuu


Comments