SEKATA YA MADINI YACHANGIA KUONGEZA MAPATO YA TAIFA


Waziri wa madini Mhe.Doto Biteko amesema sekta ya madini imechangia ongezeko la mapato kuongezeka
kutoka bilioni 196 kwa mwaka  mpaka bilioni 335 kwa mwaka
waziri Biteko ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa kimataifa wa uwekezaji

Katika sekta ya madini Tanzania Na kusema mafanikio hayo yamefikiwa baada ya wachimbaji na
wawekezaji katika sekta hiyo kutambua umuhimu wa kuuza madini katika masoko maalum yalioanzishwa hapa nchini na kuondoa vitemdo vya urasimu katika soko
la madini.

Huku waziri wa nchi anaeshughulikia maendeleo ya madini Nchini Uganda Mhe Sara Upendi akisisitiza umuhimu wa kuwa na sheria kali za kulinda rasilimali madini barani Afrika.

wakiwasilisha maoni yao kwa serikali baadhi ya wawekezaji katika sekta ya madini hapa wamesema mazingira ya kununua madini kwa sasa yamekuwa rafiki kutokana na utekelezaji wa sheria mpya pamoja na uwepo wa mikutano hiyo inawapa fursa ya
ya kutoa maoni na changamoto zinzowakabili.

kwa upande wao baadhi ya wachimbaji wadogo pamoja na idara mbali mbali zinazosimamia sekta ya madini
wakaelezea fursa za mikutano hii ya kimataifa katika kutangaza rasilimali mali madini
yanayopatikana hapanchini

Comments