Afisa Tawala Wilaya ya Bukombe Ally Mketo akizungumza na waumini wa Kanisa la Ufunuo jimbo la Geita lililopo mjini Ushirombo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba.
Askofu wa kanisa la Ufunuo jimbo la Geita, Heryyabwana Majebele akiwapaka mafuta ya utumishi wachungaji wasimikwa.
Mkuu wa Chuo cha Biblia Geita Bible Training Center (GBTC) Alexander Maningu akiwavisha kola Wachungaji 11 baada ya kuwekwa wakfu.
Wachungaji 11 wawekewa wakfu na Askofu wa Kanisa la
Ufunuo Jimbo la Geita, Heryyabwana Majebele baada ya kuhitimu masomo yao chuo cha
Biblia Geita Bible Training Center (GBTC) na kufikia daraja la uchungaji.
Askofu Majebele akiwaweka wakfu wachungaji wapya 11 aliwataka
kuacha tamaa za kidunia na kufanya kazi waliyoitiwa
na Mungu kwa kuwa mfano wa kuigwa ndani ya makanisa watakayo pewa na jamii inayo wazunguka.
“Wachungaji watano niliwavua nyadhifa baada ya kupata taarifa zisizo mpendeza Mungu kutoka kwa waumini wa makanisa nikawaita na kuwauliza juu ya fununu hizo wakakili makosa, sasa na wachungaji
ambao nawateuwa mjipange mkitenda dhambi nitawatumbua zingatieni maadili ya
kiutumishi kama mlivyo fundishwa chuoni” alisema Askofu Majebele.
Kwa upande wake Afisa Tawala wa Wilaya ya Bukombe Ally Mketo alimpongeza Askofu
Majebele kwa hatua aliyoichukuwa dhidi ya watumishi hao waliopotokwa na kusisitiza kuwa asingelikua hachukii dhambi angeliwafumbia macho
wachungaji hao wanao kiuka maadili ya ki Mungu.
Mketo alimuomba Askofu Majebele kuendelea na msimamo wake
katika kutekeleza majukumu ya kusimamia kanisa na kushirikiana na serikali kwa
kuchagia maendeleo kikamilifu.
Miongoni mwa wachugaji waliowekewa wakfu Zawadi Jemes alisema
hakutarajia kama angepata uchungaji baada ya kuhitimu masomo lakini nimpango wa
mungu kumteuwa.
Jemes alisema atahakikisha anamtumikia Mungu kikamilifu kwa
kuokoa roho zilizo potea popote atakapo tumwa na Askofu Majebele.
Comments
Post a Comment