Mkuu wa Mkoa wa Geita Robart Gabriel akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba wakishirikiana na wananchi wa Kata ya Katente kusomba mawe baada ya kuchimba msingi.
Wakazi wa Kata ya Katente wakati wa kujitolea kujenga madarasa shule ya sekondari Katente na aliye beba jiwe ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Wilaya ya Bukombe Dionis Myinga akishiriki.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Robart Gabriel ametoa wito kwa wadau wa
elimu na maendeleo Mkoani hapa kuchangia mali zao kwa kuwashika mkono wananchi
kwenye miradi ya ujenzi wa Zahanati, Vituo vya Afya na madarasa shule za msingi na
sekondari.
Gabriel alitoa wito huo wakati wauzinduzi wa kampeni ya
kumaliza upungufu wa madarasa shule za msingi na sekondari mkoani hapa
uzinduzi ikiwa uzinduzi huo ulifanyika shule ya sekondari katente ilioko Wilaya ya Bukombe kwa
kushirikiana na wananchi kuchimba msingi na kusomba mawe ili kumaliza upungufu
wa madarasa 16 shuleni hapo.
“Kampeni hii haita ishia Wilaya ya Bukombe bali ni Wilaya
zote za Mkoa wa Geita, wahakikishe wana anzisha ujenzi wa vyumba vya madarasa
shule za msingi na sekondari ili serikali ya Mkoa itafute fedha za ukamilishaji
wa vyumba vya madarasa vitakavyo jengwa
kwa nguvu za wananchi” alisema Gabriel.
Na kupitia uzinduzi huo wa kampeni ya kumaliza changamoto ya
upungufu wa madarasa kimkoa Mkuu wa Mkoa Gabriel alikusanya mifuko 200 kati ya mifuko hiyo 50 ilitolewa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko.
Mkazi wa Kata ya Katente Edward Samson alisema wameaza
kushiriki kuchimba msingi na kusogeza mawe kutokana na Mkuu wa Mkoa wa Geita Robart
Gabriel kufika na kuonyesha hamasa kubwa kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya
Bukombe Said Nkumba.
Nae Afisa Taluma shule za sekondari mkoa wa Geita Christabela
Ngatoluwa alisema shule za sekondari kwa mkoa wa Geita zipo 118 huku shule za
sekondari kidato cha tano na sita zipo 2.
Ngatoluwa alisema mahitaji ya vyumba vya madarasa ni 615
madarasa yaliyopo 398 upungufu madarasa 217 na kwamba upungufu huo kitaluma ni changamoto
kwa wanafunzi inasababisha msongamono hali ambayo inawafanya wanafunzi kutofanya
vizuri kitaluma.
Mkuu wa shule ya katente sekondari Sigano Mokiri alisema shule
inawanafunzi 1530 wasichana 731 wavulanaa 799 uhitaji wa madarasa 34 yaliyopo
18 upungufu 16 alisema kupitia hamasa ya serkali ya mkoa na wilaya wananchi
wamehamasika kujitolea kuchimba msingi vyumba
vyote ambavyo ni mapungufu ili ujenzi uanze.
Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba alisema
kutokana na moto uliowashwa na Mkuu wa Mkoa Wilayani Bukombe ni kwa nia ya dhati
kuleta maendeleo.
Nkumba aliwaomba wananchi kuendelea kujitoa nguvu zao kwa
kuchimba msingi ya madarasa na miradi mingine ikiwemo kusogeza mawe na mchanga,
na maji ili serikali inapoleta fedha zikamilishe mradi na fedha zibaki na
kuazisha miradi minginge.
Comments
Post a Comment