Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma akizungumza na Viongozi pamoja na Wananchi katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya ya Bukombe
Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma akiwa na viongozi mbalimbali wakikata utepe tayari kwa ufunguzi wa jengo jipya la Mahakama ya Wilaya Bukombe.

Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel wakifanya ufunguzi wa jengo jipya la Mahakama ya Wilaya ya Bukombe.

Muonekano wa jengo jipya la Mahakama ya Wilaya ya Bukombe.

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba akizungumza na Viongozi pamoja na Wananchi katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya ya Bukombe.
Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma amewataka watanzania kutafuta haki Mahakamani badala ya kujichukulia sheria mkononi wanapo onewa au kukamata wahalifu.

Profesa Juma ameyasema hayo wakati akifungua jengo jipya la
Mahakama ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, mjini Ushirombo.
Profesa Juma ametoa wito kwa Mahakimu na watumishi wengine wa Mahakama kutumia jengo hilo na vifaa kwa kutoa huduma bora kwa wananchi na
kuepuka vitendo vya rushwa.
Awali Mtendaji Mkuu wa Mahakama Mathias Kabundugulu akisoma taarifa
ya ujenzi wa mradi huo alisema ujenzi ulianza Februari 2018 hadi kukamilika
mradi huo wa jengo wenye ukubwa wa kilomita 168 za mraba umegarimu zaidi ya sh
859 milioni.
Kabundugulu alisema mkandarasi alisema jengo hili litawaondolea mahakimu na watumishi wengine kufanyia kazi kwenye jengo la kupewa na halmashauri hali ambayo ilikuwa ikiwapelekea kufanya kazi kwenye maeneo ya kubanana.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Bukombe Said Nkumba aliwaomba wananchi Wilayani hapo kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwenye vyombo vya Dola kuwafichua wahalifu ili wachukuliwe hatua za kisheria na sio kujichukulia sheria mkononi wanapo kamata wahalifu hao na kuwachoma moto badala yake washirikishe vyombo vya Dola kisha wawapeleke mahakamani.
Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma akiwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na viongozi wa Dini katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa jengo jipya la Mahakama ya Wilaya ya Bukombe
Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma akiwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Mahakama katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa jengo jipya la Mahakama ya Wilaya ya Bukombe
Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma akiwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa na Wilaya katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa jengo jipya la Mahakama ya Wilaya ya Bukombe
Comments
Post a Comment