Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Kata ya Iyogelo.
Diwani wa Kata ya Iyogelo Juma Lushiku akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Kata ya Iyogelo.
Diwani wa Kata ya Iyogelo akikabidhi taarifa ya utekelezaji kwa Juma Lushiku Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Bukombe ambae pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo Said Nkumba.
Diwani wa Viti maalumu Rahel Sololo akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Kata ya Iyogelo.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya
Bukombe ambae pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo Said Nkumba amewataka wenyeviti wa
vitongoji na vijiji kuhamasisha wananchi kushiriki kikamirifu kwenye miradi ya
maendeleo.
Nkumba aliyasema hayo wakati akihutubia wajumbe wa Mkutano
Mkuu wa CCM Kata ya Iyogelo .
Pia Nkumba alisema wasimamie utekelezaji wa ilani kwa mtu
mmoja mmoja kwa kuinua uchumi wao kupitia kilimo cha kisasa na kuachana na kilimo
cha mazoea kisicho na tija .
Awali Diwani wa Kata ya Iyogelo Juma Lushiku wakati akiwasilisha
utekelezaji wa ilani alianza kwa kumshukuru Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto
Mashaka Biteko kwa mchango wake mkubwa wa hali na mali katika kuhakikisha
miradi hiyo inakamilika kwa wakati.
“Nawaomba viongozi wa vitongoji na vijiji wa muda uliopita
bila kujali itikadi ya kisiasa nao wawe chachu ya kuhamasisha wananchi wahakikishe kuwa wanashiriki
kwenye miradi ya maendeleo”Alisema Lushiku.
Lushiku alisema kuna miradi 26 yenye thamani ya Tsh bilioni 1.8 iliyotekelezwa ndani ya kata
hiyo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa shule ya sekondari
Busonge uliogharimu Tsh milioni 33,miundo mbinu ya madarasa shule ya msingi
Bugando,kliniki za baba,mama na mtoto kwenye Zahanati mbili na miundo mbinu ya
umeme na barabara.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kata Mwanjia Said alisema
ili kufikia malengo ya maendeleo katika uboreshaji wa miundombinu ya madarasana
majengo ya kutolea huduma za Afya wanasiasa washirikiane ili kuhamasisha
wananchi kushiriki kwenye miradi kwa kuchagia nguvu na mali.
Nae Afisa Kilimo wa Kata hiyo Asteria Kibasa aliwaomba viongozi walio chaguliwa hivi karibuni
serikali za mitaa uhamasisha wakulima kulima mazao ya chakula na biashara kwa kufuata
ushauri wa watalamu ili waondokane na kilimo cha mazoea na kulima kilimo cha
faida ili waweweze kufanikiwa kukuza uchumi wa familia na taifa kwa ujumla.
Comments
Post a Comment