Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya
Bukombe Mkoani Geita imekutana na wadau
wa elimu na kutoa elimu juu ya fedha
zinazotolewa na serikali kila mwezi kutekeleza Elimu bure.
Afisa wa TAKUKURU Wilaya ya Bukombe toka dawati la utafiti na
uchunguzi Bosco Mwidadi alisema robo ya mwaka wafedha 2018/19 TAKUKURU
walifanya ufatiliaji kwenye miradi ya maendeleo hasa katika mpango wa fedha
zinazotolewa na serikali kutekeleza Elimu bure katika shule 10 kati ya shule
zamsingi 79.
Mwidadi alisema hayo
kwenye warsha ya wadau wa Elimu katika ukumbi
wa mikutano halmashauri ya Wilaya kilichohudhuliwa na wenyeviti wa kamati ya
maendeleo ya shule na walimu wakuu wa shule za msingi 79 na Maafisa Elimu kata
17 madiwani na wananchi, ili kujadili matokeo ya TAKUKURU waliyo ya baini kweye
ufatiliaji wa miradi ya maendeleo mashuleni.
“ TAKUKURU iligudua ukeukwaji wa maelekezo ya serikali kwenye
fedha za Elimu bure”. Alisema Mwidadi
Aliongeza kuwa fedha zinatumika bila kufuata mwongozo kuwa
asilimia 30, ukarabati asilimia 30 zinunua vifaa vya kujifunzia na kufundishia,
asilimia 20 itumike kwa ajili ya mitihani asilimia 10 kwa ajili ya utawala
asilimia 10 itumike kwa ajili ya michezo.
Mwidadi alisema fedha
za michezo zinatumika kwa wingi na za
kugharamia mtihani wa moko na ukarabati, pia upande wa manunuzi kuna shida
kubwa kwani kunaukeukwaji wa sheria za manunuzi ikiwa ni pamoja na kumbu kumbu
za manunuzi na malipo hazitunzwi hali
ambayo inasababisha shule kushindwa kumudu gharama za kujiendesha.
Alisema kabla ya TAKUKURU kuanza kuchukuwa hatua wameona
wawaite na kuwakumbusha kutunza kumbu kumbu za manunuzi na malipo.
Nae Mwenyekiti wa Walimu Wakuu Wilaya ya Bukombe Charles
Kisombi alisema ni kweli kunachangamoto kubwa katika utekelezaji wa fedha za
Elimu bure .
Kisombi alisema walimu wengi walikuwa hawazingatii miongozo
za manunuzi na malipo wakijua wako sahihi kumbe wako nje ya taratibu kutokana
na TAKUKURU kuwapa mafunzo walimu wameyapokea kwa njia chanya.
Kisombi alitoa wito kwa walimu wakuu kuzingatia sheria za
manunuzi na malipo kupitia mafunzo hayo ya TAKUKURU na kwamba walimu wakuu
wanamikakati ya kuita watalamu ili wafundishwa mifumo na sheria za manunuzi na
malipo katika utekelezaji wa Elimu bure.
Kwa pande wake Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba akitoa
taarifa ya fedha zinazo tolewa na serikali kila mwezi kutekeleza Elimu alisema
serikali tangu 2015 hadi septemba mwaka 2019 Tsh bilioni 2.12 zimepokelewa kwa
ajili ya Elimu bure shule 79 za msingi.
MWISHO
Comments
Post a Comment