SILOKA WALIMU FC WATWAA UBINGWA MWALIMU DOTO CUP 2019




Timu ya Walimu wa Tarafa ya Siloka Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita, wameibuka kidedea na kutwaa ubingwa wa kombe la Mwalimu Doto Cup 2019 katika mchezo wa fainali uliofanyika uwanja wa Ushirombo sekondari kwa kutoa kichapo cha bao 2-1 dhidi ya timu ya Bukombe Walimu fc.

Wafugaji wa timu ya Siloka Walimu fc Mwalimu Bazili Danifod dakika ya 57 goli la pili lilipachikwa na Mwalimu Gerevas Njantu dakika ya 78.

Huku Mwalimu Jeremia Chacha wa timu ya Bukombe Walimu Fc akifuga goli kwa mkwaju wa penaliti na kupata goli la kufutia machozi dakika ya 89 lililo dumu hadi kipena cha mwisho kinapulizwa.

Mratibu wa Ligi ya Mwalimu Doto Cup 2019 Domisian Kabalega alisema mashindano hayo yaliaza Septemba 25 mwaka huu kwa kushirikisha timu 17 ambazo ziliundwa kupitia walimu kila shule wenye vipaji na kucheza ngazi ya Kata hadi Tarafa.

Kabalega alisema  Mshindi wa tatu ni timu ya Butinzya Walimu fc ambayo ilipokea sh 100,000 jezi seti moja na mpira,mshindi wa pili ni timu ya Bukombe Walimu fc ambao walitwaa Tsh 200,000 na jezi seti moja mpira mmoja huku mabingwa wa mashindano hayo walijinyakulia kitita cha Tsh 300,000 na jezi seti moja mipira miwili.

Nae Mudhamini wa mashidano hayo Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Biteko wakati akimkaribisha mgeni rasmi  kukabidhi zawadi kwa mabingwa wama mashindano hayo.

Biteko alisema lengo la mashindano hayo ni kuwaunganisha walimu na kuinua vipaji vyao na kwamba hadi kufikia Novemba 2 mwaka huu yamekwishwa walimu wamejenga afya zao na kuendeleza  vipaji aliwaomba na kuwasihi wakahakikishe wanaongeza kasi ya kuibua vjipaji kwa wanafunzi mashuleni.
Kwa upande wake Waziri wa Elimu Sayasi na teknolojia Prof. Joyce Ndalichako alimpongeza Mwalimu Doto Biteko ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Waziri wa Madini kwa kitendo cha kuendelea kuwakumbuka Walimu wezake kwa kuwaunganisha ikiwa ni pamoja na kudhamini mashindano ya Mwalimu Doto Cup 2019.

Comments