PROF. NDALICHAKO AACHA NEEMA BUKOMBE Novemba 2, 2019



Waziri wa Elimu Sayasi na teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameacha neema Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita, baada ya kuahidi kuongeza nguvu za serikali Tsh milioni 100  kwa ajili ya ukamilishaji wa bwalo la wasichana katika shule ya sekondari Businda.
 
Prof. Ndalichako alitoa neema hiyo baada ya kufanya ukaguzi wa miundombinu ya shule ya sekondari Businda na kumridhisha na kuahidi kutoa Tsh milioni100 kutoka kwenye mfuko wa lipa kutokana na matokeo EP4R awamu ya nane itakayo tolewa na serikali mwishoni mwa Novemba mwaka huu.

Prof. Ndalichako alimpongeza Mbunge wa Jimbo hilo Doto Biteko kwa namna anavyoshirikiana na watalamu wa halmashauri na viongozi wa serikali kusimamia vizuri miradi ya maendeleo na fedha iliyotolewa na serikali.

Mwaka 2018 Tsh milioni 325 ililetwa Businda ili kuboresha miundomibinu  kwa lengo la kupandisha hadhi shule hiyo na kuwa na kidato cha tano na sita kwa ajili ya wasichana.Alisema Waziri Prof. Ndalichako.

 Pia aliwapongeza viongozi wa Chama Cha Walimu Tanzania CWT Wilaya ya Bukombe kwa kujenga ofisi ambayo ameliwekea jiwe la msingi na kuongeza kuwa serikali inatambua changamoto za walimu na kwamba halmashauri nchini zihakikishe zinashughulikia sitahiki za walimu wanapo pandishwa madaraja na likizo pamoja na mahitaji mengine ili waendelee kufanyakazi zao kwa ufanisi.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Biteko aliwaomba wazazi na walezi kuwekeza kwenye Elimu kwa kushirikiana na walimu ili wanafunzi wanapokuwa shuleni watumie muda mkubwa kujifunza ili wafaulu kuendelea na masomo.

Nae Katibu wa Chama Cha Walimu Tanzania Zephania Sabuni alisema ujenzi wa ofisi hiyo hadi kukamilika itagharimu sh 40 milioni mpaka kufika usawa wa renta imegharimu Tsh milioni 6  ikiwemo nguvu ya Mbunge Biteko ya tofari 1600 zenye thamani ya Tsh milioni 1.6.

Sabuni alisema itakapo kamilisha Ofisi hiyo na kuanza kutumia itawaondolea changamoto ya utoaji wa  Tsh milioni 1 kwa mwaka kwa ajili ya kulipia pango la Ofisi waliyo panga kwa sasa.


Comments