Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko na Waziri
wa Madini amehiriki kukamirisha mradi wa ujezi wa
zahanati iliyo anza kujengwa kwa nguvu za wananchi 2015.
Biteko alibainisha kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya mabati 250,mbao za kupaulia zahanati hiyo
“Wananchi wanaoanzisha miradi ya maendeleo lazima aniwaunge
mkono pale wanapofikia ili kusogeza huduma kwa wananchi”.Alisema Biteko
Wakati huohuo Biteko alitoa mifuko mia moja kwa ajili ya ujenzi wa choo cha wanafunzi katika shule ya msingi
Imalanguzu na kuwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na serikali kwa kuibuwa
miradi ya mandeleo kwa kuazisha ujezi ili wadau wa maendeleo wachangie mali zao.
Awali Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Imalanguzu Kata ya Bukombe
Yusuph Maige alisema Kijiji kina Kitongoji sita watu kwa mjibu wa sense 2012
kijiji kina watu 2491.
Maige alisema kutokana
na kutokuwepo huduma za Afya wananchi waliazicha ujenzi wa Zahanati mwaka 2015
na kuchangia sh 38 milioni na hadi kukamilika mradi huo mwaka 2021 utagharimu
sh 100 milioni.
Nae Diwani wa Kata ya Bukombe Rozalia Masokola alimshukuru
Mbunge Biteko kwa msaada wake nakuwasihi wananchi kuendelea kumuunga mkono
anapohamasisha maendeleo.
Comments
Post a Comment