Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoa wa Geita, Doto Mashaka Biteko
amewataka madiwani jimboni kwake kushirikiana na watalamu ili kukamilisha
miradi ya maendeleo yenye ubora na kwa wakati.
Biteko alitoa wito huo kwenye mradi wa ujezi wa vyumba vya
madarasa vinne vya shule ya Igulwa sekondari iliyoanza kujengwa Machi 2018 na
ikiwa malengo ni Januari mwaka 2019 shule hiyo ifunguliwe.
Biteko alisema watahakikisha mradi unakamilika ifikapo
Januari 2020 ili wanafunzi wa kidato cha kwanza waanze kutumia madarasa hayo.
Aidha Mhandisi wa Ujenzi Wilaya ya Bukombe Dominico Shilingo
aliunga mkono wito wa Mbunge na kuongeza kuwa hapa hakuna sababu ya kuchelewa
kukamilika kwa mradi huo iwapo madiwani wakitoa ushirikiano kwa watalamu kwa
kuhamasisha wananchi nao pia kujitolea nguvu zao.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
Dioniz Myinga aliomba wananchi kuendelea kushiriki kwenye miradi ya maendeleo
kwa kujitolea nguvu zao kwa kusomba kokoto, maji na mchanga ili kumuunga mkono
Mbunge anavyo jitoa kwa hali na mali na pambana kutafuta wadau wa maendeleo wasaidie
kwenye miradi Wilayani Bukombe.
Diwani wa Kata ya Igulwa Richard Mabenga alisema mradi huo utakamilika
kwa kuwa vifaa vyote vya ujezi vipo na kwamba Mbunge Biteko amechangia kiasi
kikubwa kwenye ujenzi huo
Comments
Post a Comment