Biteko alitoa wito huo kwenye ibada ya kubariki watoto chini
ya miaka mitano katika Kanisa la E.A.G.T (Kanani) Uyovu Kata ya Uyovu Tarafa ya
Siloka Wilayani Bukombe.
Biteko alisema wajibu wa mzazi ni kulea mtoto katika misingi
ya maadili mema ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu na kuongeza kuwa watoto walio na madili mazuri serikali itapunguza changamoto za vijana kujihusisha na vitendo vinavyopelekea uvunjaji wa sheria.
Katika ibada hiyo Mbunge Biteko aliwaomba wananchi kushirikiana na viongozi wa
serikali za mitaa waliopatikana kwenye uchaguzi uliofanyika Novemba 24 mwaka huu.
Kwa upande wake Mchungaji wa Kanisa la E.A.G. T (Kanani) Uyovu Yusuph Kinoja wakati akibariki watoto alisema maombi ya Baraka
kwa watoto chini ya miaka mitano yanawafanya watoto hao kukuwa katika maisha ya duniani
kwa hekima,busara pamoja na maadili ya Kimungu
.
Kinoja alimshukuru Mbunge Biteko kwa kufika kanisani hapo kushiriki ibada na kwa namna alivyo shiriki kutoa mchango wa ujenzi wa kanisa sambamba na ununuzi wa gari la mchungaj wa kanisa hilo.
Comments
Post a Comment