BITEKO AMEWAHIMIZA WAZAZI KUWEKEZA KWENYE ELIMU

 Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko amewahimiza wazazi na walezi Wilayani hapo kuwekeza mali zao kwenye Elimu kwa kusomesha watoto wao badala ya kuwapa urithi wa mali.

Biteko alitoa wito huo wakati akikabidhi vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya 20.8 milioni shule ya msingi Segwe Kata ya Ng’anzo na shule ya msingi Mwalo kata ya Ushirombo wakati wa ziara ya kwenda anahamasisha maendeleo Jimboni .

Mbunge Biteko na Waziri wa Madini katika shule ya msingi Segwe alitoa mifuko ya saruji 250  huku shule ya singi Mwalo alitoa mifuko ya saruji 123 zenye thamani ya Tsh milioni 6.9  na Tsh. laki sita kwa ajili ya ununuzi wa Kokoto na fedha tasilimu sh 9.7 milioni kwa ajili ya ununuzi wa mbao za kupaua madarasa matatu na mabati 120  yenye thamani ya Tsh  milioni 4 shule ya msingi Segwe.


Awali Mtendaji wa Kata ya Ng’anzo Asia Njalikai akibainisha yaliyofanywa na Mbunge Biteko kwa kata hiyo alisema alitoa tofali 1000 za saruji na mifuko ya saruji 50 kwa ajili ya ujenzi wa choo na kuanzisha ujenzi wa vyumba vitatu pamoja na Tsh milioni moja kwa ajili ya ukamilishaji wa nyumba za walimu shule ya msingi Kazibizyo.


Njalikai alisema hakuishia Kazibizyo tu pia aliendelea kuwashika mkono   wanachi wa Mtakuja kwa kutoa bati 190, Tsh milioni 3, mifuko 115 ya saruji kwa ajili ya ukamilishaji wa vyumba vitatu vya madarasa na Ofisi moja shule ya msingi Mtakuja pamoja na mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Sekondari ya Ng’anzo. 

Kwa upande wake Mkuu wa shule ya msingi Segwe Simon Sombi alimushukuru Mbunge Biteko kwa kuchangia hali ambayo itapunguza uhaba wa madarasa na kumhakikishia kuzidi kufanya vizuri katika mitihani ya Kitaifa licha ya changamoto walizonazo shuleni hapo.

Nae Mkuu wa shule ya msingi Mwalo Makoye Ludubala akishukuru mchango wa Mbunge Biteko  wa mifuko ya saruji 123 na Fedha Tsh. laki tatu kwa ajili ya kusomba kokoto tripu tatu.



 Mbunge wa Jimbo la Bukombe  Mkoani Geita Doto Biteko (wapili kutoka kushoto) akikagua madarasa ya shule ya msingi Segwe baada ya kukabidhi saruji. 



Mbuge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Biteko (wanne kutoka kushoto) akiwa anapiga makofi baada ya kufurahishwa jambo kwenye mkutano wa kuhamasisha maendeleo kijiji cha Segwe kata ya Ng'anzo.
  
Katibu Tarafa ya Ushirombo Wilaya ya Bukombe Lameck Murugwa akimkalibisha Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Biteko kwenye mkutano wakati wa ziara yake ya kwenda anahamasisha maendeleo.


 Diwani wa Kata ya Ng'anzo Kipara Siyantemi akielezea changamoto na mafanikio yaliyofanyika mbele ya Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko


 Mbunge wa jimbo la Bukombe Mhe Doto Biteko akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Segwe Kata ya Ng'anzo.




 Mbunge wa jimbo la Bukombe akishirikiana na viongozi mbalimbali wa Kaya Ushirombo katika uwekaji wa jiwe la msingi shule ya msingi Mwalo.




 Kikundi cha Hamasa kikitoa burudani kwenye Mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko


Diwani wa Kata ya Ushirombo Mhe Lameck Warangi akizungumza na wakazi wa Kjiji cha Mwalo kwenye mkutano ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko.


Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akijibu maswali ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara kijiji cha Mwalo kata ya Ushirombo.

Comments