Shule ya Msingi Ibambilo baada ya kuezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua.
Mwonekano wa Shule ya Msingi Ibambilo baada ya kuezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua.
Hali halisi ya choo cha wanafunzi wa kike baada kuezuliwa.
Picha ya Kanisa la Wadventista Wasabato Bulega baada ya kuezuliwa.
Diwani wa Kata ya Bulega Tarafa ya Ushirombo Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita, Erick Kagoma amewaomba wadau wa maendeleo kushirikiana na wananchi wa Kata hiyo kuongeza nguvu za haraka kwenye ujenzi wa miundo mbinu ya madarasa ya shule ya msingi Ibambilo baada ya kuezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua.
Erick aliyasema hayo wakati akizungumza na mwananchi shuleni
hapo alipofika kujionea hali ya uharibifu wa shule hiyo na baada ya nyumba za ibada
ikiwemo kanisa la waadventista Wasabato na kuwasihi
wananchi hao kuanza kujenga nyumba zenye ubora kwa kuziwekea renta
Mkuu wa Shule ya Msingi Ibambilo Magembe Shimba alisema tukio
lilitokea Oktoba 1 majira ya saa 9:00 mwaka huu kabla ya wanafunzi kutawanyika.
Shimba alisema mvua hiyo iliyoambatana na upepo mkali ilianza na kuharibu miundombinu ya vyumba vya madarasa
vinne na choo cha wanafunzi wa kike.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko aliwapa
pole wanafunzi na walimu kwa kunusurika na tukio hilo wakati huo huo alikabidhi
msaada wa Tsh milioni 1 wakati halmashauri inajipanga kuweka bajeti ya
ukamilishaji wa miundombinu ya shule hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba alitoa wito kwa
wananchi wa Bukombe kuwa makini na msimu wa mvua sambamba na kujenga tabia ya
kuitunza miti ya uoto wa asili inayo saidia majanga ya upepo.
Nkumba amewaagiza watalamu wa halmashauri kufanya haraka kufanya
tathimini ya gharama zitakazo tumika ili kuhakikisha miundo inakamilika kwa wakati.
Nkumba alitoa wito kwa wananchi kuboresha nyumba zao hasa
kuondokana na kuegeshea mabati mawe na magogojuu ya nyumba hali ambayo ni hatari kwa wakati wa
mvua ambazo zinanyesha kwa kuambatana na upepo mkali.
Comments
Post a Comment