"Naahidi laki tano kwa kila mwanafunzi atakayefaulu kwa daraja la kwanza katika mtihani wa kidato cha nne" -Mhe BITEKO


Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko ametoa ahadi ya shilingi laki tano kwa kila mwanafunzi atakayefaulu kwa daraja la kwanza katika mtihani wa kidato cha nne 2019.

Biteko alitoa ahadi hiyo Oktoba 16, 2019 kwa wahitimu wa kidato cha nne katika Shule Sekondari Busangi iliyopo Halmashauri ya Msalala, Wilaya Kahama mkoani Shinyanga alipokuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali yao.
Aidha Biteko aliahidi mifuko 300 ya saruji kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuondokana na changamoto ya uhaba wa madarasa shuleni hapo.

Comments