MFUKO WA JIMBO WA KWAMUA MIRADI 18 YA ELIMU NA AFYA

muonekano wa shule ya msingi bugerenga baada ya kupelekewa bati 93 na kukamilishwa na mfuko wa ep4r

Wajumbe wa Kamati ya Mfuko wa Jimbo wakiwa wamefika kujionea hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa shule sekondari Katome baada kutoa bati 157 kuunga mkono juhudi za wananchi.

Kwa mwaka wa fedha 2018/19 Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita imenufaika na mfuko wa Jimbo na kukwamua miradi 18 kati ya miradi hiyo ni Zahanati tano na ujenzi wa miundombinu ya shule za msingi 10 na shule za  sekondari tatu ambazo ni Butinzya ,Ng’anzo na Katome. 

Afisa Mipango Wilaya ya Bukombe Sylivia Lwehabula akizungumuzia Mfuko wa Jimbo unavyo kwamua miradi ya maendeleo Wilayani hapa kwa mwaka wa fedha 2018/19 alisema miradi 18 imepelekewa fedha Tsh milioni 19.7 huku na vifaa vya ujenzi mifuko ya saruji 400 yenye thamani ya Tsh milioni 7.4  na mabati  722 yenye thamani ya Tsh milioni 20.2 

Lwehabula alisema  mfuko huo unaosimamiwa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko  katika miradi ya maendeleo ameelekeza mfuko huo ili kuibadirisha Bukombe na kuwapunguzia wananchi michango.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Namonge Mlalu Bundala alimpongeza Mbunge kwa kuwashika mkono wananchi kila mwaka wa fedha mfuko wa Jimbo.
Bundala alisema  Mbunge Biteko mbali na Mfuko wa Jimbo amekuwa akichangia fedha na vifaa vya ujenzi sambamba na vifaa vya michezo akiwa katika ziara zake za kuhamasisha maendeleo kwa wananchi


Nao Wakazi wa Mjni Ushirombo Abubakari Msita alisema Mbunge asichoke kuweka nguvu za Jimbo kwenye miradi kutokana na wananchi kukosa michango kwa wakati hali ambayo inapelekea miradi mingi kusimama katika hatua ya msingi.


Latifa Gabriel aliomba halmashauri kuhakikisha wanakamilisha miradi ambayo iliazishwa na wananchi na kuongezwa nguvu na Mbunge ili ianze kutoa huduma kwa wananchi hasa Zahanati na Vituo vya Afya.

Comments