Wakugombea nafasi za uenyekiti wa vitongoji kutoka Kata ya Katente kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi wakiwa wamefika kwa
Mkurugenzi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Katentekwa ajili ya uchukuaji wa fomu.
Mkurugenzi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Katentekwa ajili ya uchukuaji wa fomu.
Mkurugenzi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Katente
Issa Shaaban akitoa maelekezo kwa wagombea waliofika kuchukua fomu za kugombea nafasi za uenyekiti wa vitongoji kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi
Wakugombea nafasi za uenyekiti wa vitongoji kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi wakiwa katika Ofisi ya chama chao kwa ajili ya zoezi la kujaza fomu za kugombea.
Mgombea uenyekiti kitongoji cha majengo Elizabeth Mwenda akirejesha fomu ya kugombea nafasi ya uenyekiti
Mgombea uenyekiti ktongoji cha bomani Ndugu Bundala Ngavune akirudisha fomu kwa msimamizi msaidi wa uchaguzi kata ya katente
Mgombea uenyekiti kitongoji cha kitangili Cosmas Pobobo Machibya akitoa mkono wa shukrani kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Katente
Issa Shaaban kwa niaba ya wenzake
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Wilaya ya Bukombe Ladislaus
Soku alisema Wilaya ya Bukombe ina
vitongoji 348 vijiji vya uchaguzi 64 Kata
17 Tarafa tatu na kuwahakikishia ushindi wa gombea kupitia CCM baada ya kujipanga na uchaguzi kikamilifu kwa asilimia 99 wanauhakika wa ushindi vitongoji na vijiji
vyote.
Nae Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Kata ya Katente Eligius
Nyabwisho alisema Kata ina mitaa mitano wagombea wako watano na kwamba CCM
imejipanga kuhakikisha wagombea wanashinda.
Mgombea Kitongoji cha Majengo Elizabeti Mwenda alisema kazi aliyo
nayo ni kutetea kiti chake kwa wananchi kwani tangu 2014 alishinda na kwamba
Chama Cha Mapinduzi CCM kimemwamini tena.
“Wananchi waliniamini na sasa wananiamini nitashinda”Alisema
Mama Mwenda.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Katente
Issa Shaaban alisema Kata ina vitongoji
vitano na wamefika wagombea watano kuchukuwa fomu na kurudisha saa 6:20 mchana huku wagombea
watano kwa tiketi ya Chadema wamefika na kuchukuwa fomu lakini hawaja rudisha.
Shaban alisema wanategemea wagombea kuja kuchukuwa fomu toka
vyama vya siasa vinne CCM, CHADEMA, CUF, ACT wazalendo na mwisho wa kuchukuwa
fomu na kurudisha ni Novemba 7 mwaka 2019.
Shaban alitoa wito kwa wagombea na viongozi wa vyama vya
siasa kufuata sheria,kanuni na miongozo
iliyotolewa na tume ya uchaguzi kupitia mkurugenzi wa uchaguzi ngazi ya Wilaya
alieteuliwa na Waziri mwenye dhamana ili kamati za madili zisipate kazi sana
katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2019.
Comments
Post a Comment