Waziri wa Nishati Dk Medard Kareman
amemsimamisha kazi Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Wilaya ya
Bukombe Mkoani Geita, Thadey Mapunda kwa kutoridhishwa na utendaji kazi wake kwa
kushindwa kusambaza nguzo na kuwasha umeme wa Rea awamu ya tatu kwa wakati na
kutoza wananchi fedha za nguzo kinyume na maelekezo ya serikali ya mwananchi kununua nguzo za umeme.
Dk Karemani alimsimamisha kazi meneja
huyo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Kapela Kata ya Igulwa Wilayani
hapa baada ya Waziri kupitia maeneo ya stendi ya mabasi kukuta hakuna umeme na
kutoka mjini Ushirombo kwenda mtaa wa Magorofani nguzo zimechimbiwa jana huku
meneja akimdanganya kuwa nguzo hizo zina zaidi ya mwezi zimesimama.
“Nimekuja Bukombe mara tatu na kutoa
maagizo lakini bado kuna malalamiko makubwa kwa wananchi wanataka umeme, sasa ifikie
mwisho maana kabla ya kufika hapa kiwanjani nimefanya ukaguzi mdogo nimepita
soko kuu na stendi ya mabasi hakuna umeme wakati ni swala la kutatuliwa siku
moja.
"Nimetoa maelekezo kesho
septemba 15 iwekwe transfoma ili umeme uanze kuwaka na nimeenda mtaa wa kapela
kuna nyumba nzuri lakini hazina umeme nifedheha kubwa sana harafu namuuliza Meneja
nguzo amechimbia lini ananijibu mwezi jana huku zinaonekana amechimbia jana au
leo asubuhi baada ya kusikia nakuja sijalidhishwa na utendaji kazi wa meneja
tanesco Wilaya na naangiza kuanzia sasa namsimamisha kazi asionekane hata
kwenye msafara wangu na kesho meneja wa Mkoa leta Meneja mwingine hapa hakuna
mwananchi kutozwa zaidi ya sh 27000 na hakuna kununua nguzo kama kuna Meneja
anauza nguzo ajifute kazi”alisema Dk Karemani.
Dk Karemani alitowa maelekezo kwa Meneja
wa Tanesco Mkoa wa Geita Joachim Ruweta na Mkandaras wa Mradi Bakari Abdallah
kwa kushirikiana na Meneja wa Kanda Maclean Mbonile siku 30 mradi uwe umefika kijiji
cha Nipha, Majengo,Kelezia,
Magorofani,stendi kuu ya mabasi pamoja na maeneo mengine ambayo hayajafikiwa na
umeme.
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba
akitoa taarifa ya mradi wa Rea awamu ya tatu alisema mradi huo utafika kwenye
vitongoji 348 na vijiji 70 vya kiumeme ndani ya kata 17 na unatekelezwa na
mkandarasi aitwaye whitecityguangdong jv
ltd mradi ulianza kutekelezwa wilayani hapa Januari 2018 na utakamilika mwaka 2020 utagarimu
sh14.8 bilioni wateja wapatao 406 wamesha unganishiwa umeme na nguzo
zimefikishwa kilomita 196 kati ya hizo nguzo kilomita 31.20 waya umevutwa.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto
Biteko alisema iwapo umeme utafika kwa wananchi kwa wakati itawafanya kuwa na
fursa za kujiajiri na kupandisha uchumi wa familia zao na Taifa.
Biteko alisema kuna vijiji ambavyo
vilishasahaulika viko Kata ya Uyovu ikiwemo Kijiji cha Kanembwa na kumuomba Waziri
wa Nishati kuona umuhimu wa kufikisha mradi huo ili wananchi wafanye kazi za
uzalishaji mali kwa kuanzisha viwanda vidogovidogo katika maeneo yao.
Mkandaras wa mradi huo toka kampuni
ya whitecityguangdong jv ltd Baraka
Abdallah alimuhakikishia Waziri wa Nishati
kuwa ifikapo Desemba mwaka huu atakuwa amekamirisha Mradi.
Comments
Post a Comment