WALIMU KATENTE FC KUENDELEA KUBAKI KILELENI KWENYE MICHUANO YA MWALIMU DOTO CUP 2019


Ikiwa ni mwendelezo wa mashindano ya  Ligi ya mwalimu Doto cup 2019 katika Viwanja mbalimbali Wilayani Bukombe Mkoa wa Geita. 



Timu ya Walimu Bulangwa fc ilikubali kupigwa bao tano toka kwa wachezaji wa timu ya Walimu Katente Samwel Marco dakika ya 12 na 14 Elias Kiondo dakika ya 17 Mwalyoyo Antony dakika ya 32 Busanya Renatus dakika ya 36.



Wafugaji wa magoli ya timu ya walimu Bulangwa Lameck Moja dajika ya 8 goli la pili lilifunga na Agustino Sonda dakika ya 86 hadi kupenga cha mwisho.



Upande wa Mchezo wa mpira wa pete bado mabingwa waliendelea kusalia walewale Walimu wa Katende baada ya kumimina kipigo cha gori 21 huku mahasimu wao ambao ni Walimu wa Bulangwa wakiambulia gori 10



Kocha wa timu ya walimu Katente fc Dionise Nkwabi alisema ushindi huu walisitahili kuupata kutokana na kujipanga kimazoezi na kwamba ubingwa wa ligi ya Mwalimu Doto Cup 2019 wata twaa ubingwa na kusisiza kuwa timu inayo pangwa kucheza mchezo unaofuata watarajie kupokea kipigo cha mabao ya kutosha.


Kocha wa timu ya Mwalimu Bulangwa Fc Freck Mshana ameleeza mapokeo yake kwa mechi ya leo kuwa  wamecheza vizuri lakini hatukufanikiwa kupata ushindi na kuahidi  timu kuendelea kuinoa ili mashindano mengine wafanye vizuri.



Kutoka katika viwanja vya Bukombe Timu ya Walimu Lyambamgongo  Fc iliibuka kidedea kwa kuichapa gori 3-0 dhidi ya Timu ya Mwalimu Bukombe Fc. 


Comments