“Vijana undeni vikundi ili kunufaika na asilimia nne za Halmashauri”MWENYEKITI WA UVCCM BUKOMBE

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana Ccm Wilaya ya Bukombe Nelvin Salabaga akuzungumza na wanafunzi ambao ni wanamichezo wa Shule ya Sekondari Runzewe.
 
Katibu Jumuiya ya Vijana Ccm Wilaya ya Bukombe Philibert Ngemela akitoa salamu kwa vijana wanamichezo wa Shule ya Sekondari Runzewe (hawapo pichani).

 
 Katibu wa Hamasa na Chipukizi Jumuiya ya Vijana Ccm Wilaya ya Bukombe Johari Kivia akitoa nasaha kwa vijana wanamichezo wa Shule ya Sekondari Runzewe (hawapo pichani). 

  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana Ccm Wilaya ya Bukombe Nelvin Salabaga akimkabidhi jezi nahodha wa timu ya Shule ya Sekondari Runzewe. 


  Uongozi wa  Jumuiya ya Vijana Ccm Wilaya ya Bukombe,wajumbe wa baraza hilo wakiwa na   wanafunzi ambao ni wanamichezo wa Shule ya Sekondari Runzewe katika picha ya pamoja.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana Ccm Wilaya ya Bukombe Nelvin Salabaga akimkabidhi jezi nahodha wa timu ya Shule ya Sekondari Uyovu. 




  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana Ccm Wilaya ya Bukombe Nelvin Salabaga akuzungumza na wajumbe wa baraza maalum la vijana Wilaya lililofanyika katika Ofisi za CCM Kata ya Uyovu.

 
 Wajumbe wa Baraza maalum la Vijana

Mkuu wa Wilaya Bukombe Said Nkumba akizungumza na Wajumbe wa Baraza maalum la Vijana Wilaya ya Bukombe.





Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana Ccm Wilaya ya Bukombe Nelvin Salabaga amewataka Vijana kuwa mstari wa mbele  kuunda vikundi vya ujasiriamali ili kunufaika na mikopo inayotolewa kwa vijana kila mwaka wa fedha na Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe.

Salabaga alitoa wito huo wakati akihutubia baraza la vijana (Uvccm) lililofanyika Kata ya Uyovu Tarafa ya Siloka Wilayani hapa.

Alisema iwapo vijana watachangamkia fursa hiyo ya mkopo na kuifanyia kazi kwenye miradi na sio kuzichezea fedha kwa kujiingiza kwenye starehe wataweza kujikwamua kiuchumi kwa mtu mmojammoja na jamii nzima kwa ujumla. 

Katika ziara hiyo Salabaga alitembelea Shule ya Sekondari ya Runzewe na Uyovu na kuzungumza na wanafunzi ambao ni wanamichezo wa shule hizo na kuwakabidhi jezi za michezo zilizotoka kwenye Ofisi ya Mbunge Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko.
   
Awali Mwenyeti wa Jumuiya ya Vijana Ccm kata ya Uyovu wakati akimkaribisha Mwenyekiti wa Wilaya alianza kwa kumpongeza  kwa kazi anazozifanya za kuijenga jumuiya hiyo na kuwafanya vijana kuwa wamoja.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Bukombe Said Nkumba aliwataka vijana kutokubeza wito wa Mwenyekiti wao wa Wilaya ili kunufaika na Serikali.

Nkumba aliwataka Vijana kuchangamkia fursa ya kugombea uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwaka huu na kutokutumiwa vibaya na katika uchaguzi huo kwa maslahi ya mtu binafsi na kusahau uzalendo wanchi.

Comments