Mbunge
wa Viti Maalum Mkoa wa Geita Mhe. Josephina Chagulla akizungumza na wajumbe wa Jumuiya ya wanawake Ccm Wilaya ya Bukombe
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake Ccm Wilaya ya Bukombe Agnes Sayi akionyesha furaha za ujio wa Mbunge huyo na kufungua mkutano huo.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Geita Safia Bakari akizungumza na Jumuiya ya wanawake Ccm Wilaya ya Bukombe
Mkurugenzi wa Kampuni ya open mind and though
organizasion (OMTO) Anna Haule akitoa somo la ujasiriamali.
Mmoja wa Wakufunzi akitoa mada kwa furaha kabisa.
Wajumbe wa UWT Wilaya ya Bukombe wakiwa katika mapokeo.
Jumuiya ya wanawake Ccm Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita imenufaika
na elimu ya Ujasiriamali iliyotolewa na wakufunzi waliokuwa wameambatana na Mbunge
wa Viti Maalum Mkoani hapa Josephina Chagulla
Chagulla kabla ya kuwakaribisha watalamu wa mafunzo ya
ujasiriamali kuzungumza na wamama hao alisema wanawake wajasiriamali Mkoani
hapa wanamitaji lakini hawana utalamu wa kuongeza thamani ya bidhaa kwa kuweka
kwenye vifungashio vilivyo katika ubora.
Alisema kupitia mafunzo hayo ambayo watayapata yatawasaidia
kuwa wa bunifu na kuongeza thamani ya bidhaa na kuwahakikishia upande wa
changamoto ya soko la bidhaa zao na ukosefu wa vifungashio ataweka mikakati na
wadau ili kuwa na kiwanda kidogo cha kutengeneza vifungashio vyenye ubora.
Upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya open mind and though
organizasion (OMTO) Anna Haule alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwafanya wanawake
kujitambua ili kujikwamua kiuchumi ili wafanye siasa wakiwa na uchumi.
Nae Mkurugenzi wa shirika
la Road-to-success Rodrick Nabe aliwataka
wanawake viongozi wa UWT ngazi ya Kata kutoa hamasa ya wanawake kujiunga katika
vikundi na kuanzisha ujasiriamali.
Akieleza mjasiriamali ambae
pia ni mwenyekiti wa UWT Kata ya Bulega Rahabu Ngukulu kwenye mafunzo ya
ujasiriamali yaliyokuwa yanatolewa kwa wenyeviti na makatibu wa UWT kata zote
17 za Wilaya ya Bukombe ambayo ni namna ya kutengeneza pafyumu,pilipili sosi, Sabuni ya
mche kwa kutumia mchele.
Ngukulu alisema
wanawake wengi wamekuwa wakishindwa kuazisha ujasiriamali kutokana na maisha
duni na kuwa tegemezi kwa wanaume kuendesha familia.
Pia Elizabeth Paul alisema mafunzo hayo ya ujasiriamali
yamempa mwanga na kufikiri kuboresha biashara yake ya kutengeneza sabuni ya
kufulia kwa kutumia mchele.
Wakati huo huo Mbunge Chagulla alikabidhi msaada wa shuka 100
kwa ajili ya wodi ya wazazi ya mama na mtoto katika hospitali ya Wilaya ya Bukombe.
Comments
Post a Comment