Serikali
imefuta vibali vyote vilivyokuwa vimetolewa kwa wafanyabiashara wa
vyuma chakavu na biashara taka hatarishi kwa ujumla bila kufuata sheria
na kuagiza mchakato wa utoaji vibali hivyo uanze upya ili kuhakikisha
sheria ya mazingira inafuatwa.
Tamko
hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mhe. George Simbachawene wakati wa Mkutano na wafanyabiashara
wa vyuma chakavu uliofanyika jana Septemba 4, 2019 jijini Dar es
Salaam.
Kutokana
na hatua hiyo Mhe. Simbachawene amemugiza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu
wa Rais kuunda haraka timu ya wataalamu kutoka Baraza la Taifa la
Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa
vibali vyote pamoja na vyuma chakavu vilivyokusanywa.
Alifafanua
kuwa vibali vingine vimekuwa changamoto lukuki zikiwemo kutojulikana
ukaguzi wake au kutumika kwa zaidi ya biashara moja jambo ambalo
limekuwa likiikosesha mapato Serikali.
"Serikali
hii ya wanyonge haina nia ya kumkomoa mtu katika hili la chuma chakavu
tunawajali sana na ni biashara nzuri lakini ifikie kipindi tufuate
utaratibu na kuwa na kibali maana tumebaini kuna dosari nyingi katika
vibali vingi vilivyotolewa," alisema.
Aidha
kwa upande mwingine Mhe. Simbachawene alitangaza kuwa Serikali
imerekebisha tozo ya vyuma chakavu ya sh. milioni 10 iliyokuwa
inalalamikiwa na wafanyabiashara hao hasa wadogo na kufikia sh. milioni 5
hadi sh. laki 5.
Mhe.
Simbachawene abainisha kuwa tozo hizo ni takwa la kisheria na haliwezi
kujadiliwa au kubadilishwa hadi sheria ipelekwe Bungeni kujadili hivyo
haitawezekana kuiondoa na kuwa Ofisi hiyo inaendelea kusimamia.
Awali
akizungumza Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Samuel Gwamaka alisema kuwa
lengo la hafua hiyo ni kurasimisha baishara ya chuma chakavu na
kuwatofautisha wafanyabiashara wadogo na wakubwa ili kuwatengenezea
mazingira mazuri.
Dkt.
Gwamaka alifafanua alibainisha kuwa mfanyabiashara anapowasilisha ombi
lake NEMC wanakagua na kuwasilisha Ofisi ya Makamu wa Rais ambayo
ikijiridhishe inaliwasilisha kwa Waziri wa Nchi ambaye nae akianatoa
kibali ndani ya siku 14.
"Hapo
nyuma NEMC haikuhusika sana na masuala ya chuma chakavu lakini Waziri
alitoa maelekezo na Baraza kuanza kusimamia utekelezaji wake wa kanuni
za taka hatarishi na chuma chakavu
Comments
Post a Comment