Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana
wa CCM Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita, Nelvin Salabaga amempongeza Mbunge wa Jimbo
hilo ambae pia ni Waziri wa Madini Mhe. Doto Mashaka Biteko kwa kutoa Mifuko 50
ya saruji yenye thamani ya Tsh milioni 1 kwa ajili ya ujenzi wa choo cha
wanafunzi shule ya msingi Nampangwe.
Salabaga aliyasema hayo wakati
akizungmuza na wajumbe wa halmashauri kuu ya ccm kata ya Runzewe Mashariki
baada ya kupata taarifa za Mbunge huyo kutoka kwa Katibu wa Ccm Kata hiyo kuwa Mbunge
anashiriki kikamilifu kwenye miradi ya maendeleo inayo anzishwa na wananchi na
miradi mingine kuwezesha bila nguvu za wananchi.
“Mhe. Biteko alitoa Tsh milioni 6 kujenga
Zahanati ya Ikuzi, Tsh milioni 3 kwa ajili ya ukamilishaji wa madarasa shule ya
Sekondari Msonga huku mifuko 100 ya saruji shule ya msingi Bulumbaga” Alisema Salabaga.
Salabaga aliongeza kuwa Mbunge huyo
ni kiongizi anae tambua uwajibikaji wa nafasi yake ya uwakilishi kwa wananchi
na kutekeleza ilani ya ccm na kwamba amekuwa akijitoa michango mingi ya kuwaunga
mkono wananchi wanaokuwa tayari kujiletea maendeleo.
Kwa nyakati tofauti Salabaga akiwa
kata ya Butinzya akiwa anazungumza kwenye Halmashauri Kuu ya Ccm Kata alikuta Mhe.
Biteko amechagia Tsh milioni 5 shule ya msingi Mbula na mifuko 100 ya saruji
kwa ajiri ya ukarabati wa madarasa 4 na ofisi ya utawala shule ya msingi Ngita
huku katika shule ya msingi Mbula Mbuge alitoa Tsh milioni 4 .5 kwa ajili ya kupaua
na kukamilisha majengo ya shule hiyo.
Salabaga aliendelea kumwaga sifa za Mbunge
huyo kuwa katika ukamilishaji wa madarasa shule ya msingi Isemabuna Mhe. Biteko
alichangia Tsh milioni 2.5 huku Zahanati ya Butinza alitoa mifuko 100 ya saruji
ili kuunga mkono nguvu za wananchi na Kijiji cha Silamila kwenye ujenzi
Zahanati amechangia Tsh milioni 3.
Mbunge Biteko akizungumuza na blog ya
Bukombesasa kwa njia ya simu akiwa
Dodoma Bungeni Mhe. Biteko alisema lengo lake la kuunga mkono nguvu za wananchi
ni kuwa na dira ya kuibadilisha Bukombe.
Biteko aliongeza kuwa atahakikisha
anaendelea kuwaunga mkono viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya chini wa nao
hamasisha miradi ya maendeleo ili kuleta mabadiliko ya kimaendeleo Wilayani
Bukombe.
Diwani wa Kata ya Butinzya Mhe. Amos
Shimo akizungumuza yake toka moyoni alimpongeza Mbunge Biteko kwa kumpa
kilomita nyingi za kufungua barabara mpya za kuunganisha Kijiji cha Butinzya,Mubula
hadi Igwamanoni na Butinzya,Ngita, hadi Kata
ya Ng’anzo.
Shimo alisema nguvu za Mbunge Biteko ameziona pia kwenye kukamilisha kwa
kupaua maboma yote ya madara ya shule ya msingi na sekondari yaliyokuwa yamekwa
kwa muda mrefu hapo Katani.
Comments
Post a Comment