Mwalimu Doto Cup 2019 yaanza kutimua Vumbi




Mgeni rasmi katika ufunguzi huo Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania CWT Mkoa wa Geita John Kafimbi

Ligi ya mwalimu Doto cup 2019 yaanza kutimua vumbi Wilayani Bukombe Mkoa wa Geita huku  timu ya Walimu Ushirombo fc imewachapa bao 4-1 Timu ya Walimu Igulwa fc katika mashindano ya ufunguzi wa Ligi ya Mwalimu Doto Cup 2019 katika uwanja wa Ushirombo Sekondari.


Wafugaji wa Timu ya Walimu Ushirombo fc ni Mwalimu Medisoni Mwaipopo dakika ya 34 na 44 goli la tatu Mwalimu Mjuni Mulugo alitupia dakika ya 57  huku Bahati Kasante dakika ya 68.




Mfugaji wa Timu ya Walimu Igulwa fc Mwalimu George Mbawala   aliwapatiwa bao la kufutia machozi Walimu wezeka dakika ya 85.
Huku katika mchuano wa Mwalimu Doto Cup katika       Uwanja wa Bufanka  kati ya Walimu Bugelenga fc  4-3 dhidi ya timu ya Walimu Iyogelo fc kwa mikwaju ya penaliti baada ya kutoka sale dakika 90 ikiwa timu ya Walimu Bugelenga imefuzu kusonga mbele.






Mgeni rasmi katika ufunguzi huo Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania CWT Mkoa wa Geita John Kafimbi amesema lengo la michezo hiyo ni kuwaunganishwa walimu na kusisitiza kuwa kitendo alicho kifanya Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Mashaka Biteko kuazisha Ligi ya Mwalimu Doto Cup ni jambo jema alilolifanya la kuwakumbuka walimu wezake.
Kafimbi ameongeza kuwa michezo ni Afya na fursa ya kupata marafiki wapya pamoja na  kuongeza uimarishaji wa vipaji mashuleni.



















Comments