Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita Mhe. Doto M. Biteko amewaomba viongozi wa madhehebu ya dini kuhamasisha
wananchi kuwekeza kwenye Elimu ya watoto wao.
Biteko aliyasema hayo kwenye hafla ya
harambee ya kuchangia michango ya hiyari kwa ajili ya ununuzi wa vyombo vya muziki Kanisa la Afirican Inlad Church A.I.C Ushirombo Wilaya ya Bukombe.
“Ili kunufaika na Umoja wa Afrika Mashariki
inayoundwa na Nchi 5 pamoja na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi 16 za Kusini mwa Afrika
(SADC) ambao Mwenyekiti wake kwa sasa ni Rais Dk. John Magufuli inatakiwa wananchi wa Wilaya
ya Bukombe kuwekeza kwenye Elimu na si vinginevyo ili kuwanusuru watoto wao kuwa
watumwa wa wageni ” alisema Biteko.
Biteko akikabidhi Tsh milioni 1 kwa ajili
ya changizo la ununuzi wa vyombo vya mziki kanisani hapo, aliwaomba wananchi kila
mtu kwa imani yake aendelee kumuombea Rais
Magufuli na wasaidizi wake ili Mungu Aendelee kuwapa hekima busara na maarifa
zaidi waendelee kulitumikia Taifa letu.
Kwa upande wake Mchungaji wa Kanisa la Afirican Inland
Church (A.I.C Adamu Nzoka alisema wananchi
kwa sasa wamekua na mwamko wa kusomesha watoto wao kutokana na serikali ya awamu ya tano
kutoa Elimu Bure kuanzia darasa la awali hadi kidato cha Nne.
Nae muumini wa kanisa hilo Yohana Kasongi
alisema Elimu ambayo imetolewa na Mbunge nihamasa ambayo itasaidia wananchi
kufikisha ujumbe kwenye jami ili wawekeze kwenye Elimu.
Comments
Post a Comment