MAKATIBU WENEZI CHADEMA BUKOMBE WAENDELEA KUTIMUKIA CCM

 Mwenyekiti wa CCM Wilaya Bukombe Daniel Machongo akimkabidhi kadi ya chama hicho aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chadema Wilaya ya Bukombe Mwajuma Shabani.

Katibu wa CCM Wilaya Bukombe Tabu Lugwesa akimkaribisha CCM aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chadema Wilaya ya Bukombe Mwajuma Shabani baada ya kukabidhiwa kadi ya CCM na Mwenyekiti.
 

  Mbele wakiwa ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya Bukombe Daniel Machongo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Wilaya ya Bukombe Ladslous Soku wakiwa na Viongozi mbalimbali wa Chama hicho baada ya kumpokea rasmi  aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chadema Wilaya ya Bukombe Mwajuma Shabani.

 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Wilaya ya Bukombe Ladslous Soku kisisitiza juu ya uimarishaji wa ngome ya CCM.




Makatibu wa siasa na uenezi wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Ngazi ya Wilaya Wilayani Bukombe Mkoa wa Geita, wamehamia Chama Cha Mapinduzi CCM kwa muda mfupi wa siku 31 na kufikia viongozi wawili kutimkia CCM. 

Katibu mwenezi wa CHADEMA wilaya ya Bukombe wa kwanza Juma Maliseli alihamia CCM Agost 22 mwaka 2019 na kuchukuliwa nafasi hiyo na Mwajuma Shabani aliyehamia CCM Septemba 23.

Upande wake Mwajuma Shabani baada ya kukabidhiwa kadi ya CCM alisema amehamia chama tawala bila kushawishiwa na  kilichomufanya kwenda CCM ni kutokana na kazi za kutetea wanyonge na maendeleo yanayo fanywa Rais John Magufuli pamoja na wasaidizi wake.

“Huu ni muda wa kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano kutokana na mambo makubwa ambayo yalikuwa yana pigiwa kelele na vyama vya upinzani  na sasa yanatekelezwa na serikali ya CCM kwa kasi kubwa” alisema Shabani.

Katibu wa Itikadi na Uenezi  CCM Wilaya ya Bukombe Ladslaus Soku alisema kupitia mikakati ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2020 CCM imeendelea kubomoa ngome ya CHADEMA.
  
Soku alitoa wito kwa viongozi wa CHADEMA wanao hamia CCM kwa hiyali yao kuzingatia maadiri ya chama na kuhakikia wanalinda ilani na katiba ya nchi kuhakikisha wanadumisha amani, na mshikamano wa chama.


Comments