KIKUNDI CHA TUMAINI KUANZA KUNUFAIKA


Mwenyekiti wa Ccm Wilaya ya Bukombe Daniel Machongo akisaini kwenye kitabu cha wageni baada ya kuwasiri kwenye eneo la mradi.
 
Mmoja wa wanakikundi wa TUMAINI akisalimiana na Katibu wa Itikadi na uenezi wa Wilaya ya Bukombe Radslous Soku baada ya kuwasili.
 
Katibu wa Kikundi cha Tumaini Peter Manamba  akisoma taarifa ya mradi  kwa wajumbe wa Kamati ya Siasa ikiongozwa na Mwenyekiti wa Ccm Wilaya  ya Bukombe Daniel Machongo.

Mwenyekiti wa Ccm Wilaya  ya Bukombe Daniel Machongo akifuatilia kwa karibu taarifa ya mradi wa Kikundi cha TUMAINI.



Mwenyekiti wa Ccm Wilaya  ya Bukombe Daniel Machongo akizungumza na wanakikundi wa TUMAINI.


Wadau aliofika katika ukaguzi huo wa mradi uliofanywa na Kamati ya Siasa(Ccm) Wilaya  ya Bukombe





 Picha ya Mradi wa Kikundi cha Tumaini.


Wajumbe wa Kamati ya Siasa ikiongozwa na Mwenyekiti wa Ccm Wilaya  ya Bukombe Daniel Machongo wakijionea ufanyaji kazi wa Mashine hizo.





Kikundi cha watu wenye ulemavu (TUMAINI) kilifanikiwa kupewa mkopo wa milioni 12.2 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe na kuanzisha mradi wa mashine ya kukoboa na kusaga nafaka ili kuongeza thamani ya mazao hayo.

Hayo yalielezwa na  Katibu wa kikundi hicho Peter Manamba wakati akitoa taarifa ya mradi  uliokuwa ukikaguliwa na kamati ya siasa ikiongozwa na Mwenyekiti wa Ccm Wilaya  ya Bukombe Daniel Machongo.

Manamba alisema kikundi kilianzishwa na wajasiliamali sita,nakusajiriwa Februaari 25 mwaka 2019 ,kwa sasa kinamiliki kiwanda kidogo cha uchakataji na ununuzi wa nafaka za mazao ya chakula. Walianza na mtaji wa sh 500,000 kabla ya halmashauri kuwapa mkopo wa sh 12.2 milioni.

Kwa upande wake Mratibu wa dawati la uwezeshaji wananchi kiuchumi na kusimamia vikundi vya vijana  na watu wenye ulemavu, Ofisi ya Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Bukombe Mariana Genya alisema kikundi hicho ni miongoni mwa vikundi vitano vya watu wenye ulemavu ambavyo kwa mwaka wa fedha 2018/19 halmashauri ilivikopeshwa jumla ya Tsh milioni 17.

“Halmashauri kupitia Ofisi ya Maendeleo ya Jamii imeweza kutoa Elimu ya ujasiliamali na usimamizi wa biashara kwa wanakikundi, ili waendeshe mradi huo kama soko la ajira ,kuongeza thamani ya  mazao, kujiongezea kipato kwa wanakikundi, kuongeza mzunguko wa biashara na uzalishaji mali" Alisema Genya.

Mwenyekiti wa Ccm Wilaya ya Bukombe Daniel Machongo aliwaomba wanakikundi, kusimamia vema mradi na kurejesha mkopo  kwa wakati ili vikundi vingine vikopeshwe.

Nae Diwani wa Kata ya Bulangwa Yusuph Mohamed ambako uliko mradi huo aliwataka kutunza miundombinu ya mradi na kuhakikisha  utakapo anza kufanya kazi, watoe fursa za ajira kwa vijana na wanawake ili kuinua uchumi kwenye jamii.







Comments