HALMASHAURI KUANZA UJENZI WA LAMI YA RAIS MAGUFULI


Afisa Tawala Wilaya ya Bukombe Ally Mketo akizungumza na waumini wa Kanisa la Ufunuo Mjini Ushirombo.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Dioniz Myinga akizungumza na waumini wa Kanisa la Ufunuo Mjini Ushirombo.

Afisa Tawala Wilaya ya Bukombe Ally Mketo(mwenye tai),Katibu wa Mbunge Jimbo la Bukombe Benjamini Mgeta(mwenye kaunda suit) na Askofu wa Kanisa la Ufunuo Jimbo la Geita.
Meza Kuu.

Kwaya ya Lango la Uzima wakitoa mahubiri kwa njia ya uimbaji  



Huduma ya maombezi ikiendelea katika Kanisa la Ufunuo Mji wa Ushirombo







Utekelezaji wa ujenzi wa barabara  ya kwanza ya  lami katika halmashauri ya wilaya ya Bukombe mkoani Geita, katika bajeti ya mwaka wa fedha 2019/20 itaanza utekelezaji ahadi ya Ras Dk John Magufuli aliyotowa mwaka 2015 wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu aliahidi kilomita tano za lami mjini Ushirombo serikali imesha toa Tsh milioni 500 ziko hatua ya ununuzi ili kuanza ujenzi wa kilomita moja ya barabara ya lami kati ya tano za Rais.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Dioniz Myinga aliyasema hayo kwenye ibada ya kuombea amani,uchaguzi wa serikali za mitaa,pamoja na kumpongeza Rais Dk John Magufuli kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi 16 za Kusini mwa Afrika (Sadec) katika la kanisa la Ufunuo mjini Ushirombo.

Alisema kwa sasa halmashauri inatekeleza mradi ujezi wa barabara ya lami kilomita moja  tangu Novemba 2018 ulitakiwa kukamilika Juni 26 mwaka 2019 lakini mkandarasi anasua sua pia kuna kilomita mbili zinatalajiwa kujengwa kwa lami serikali imetenga zaidi ya Tsh milioni 950 kufuatia hali hiyo mji wa Ushirombo utakuwa na barabara ya mtandao wa lami kiliomita nne zikiwemo za Rais Dk Magufuli itakuwa lami ya kwanza tangu 1995 Wilaya kuanzishwa.

 Pia kwa bajeti ya mwaka 2019/20  halimashauri imetenga sh 1.6 bilioni kwa ajiri ya ujenzi na ukarabati barabara kiwango cha changalawe  jumla na ukarabati urefu wa  kilomita 83.2 huku halmashauri ikiwa na mtandao wa barabara yenye urefu wa barabara kilomita 1400  serikali imeizinisha Tsh milioni 600.5 toka mfuko wa maendeleo ili kuanza ujezi na ukarabati wa barabara hizo za pembeni ya mji.

Askofu wa Kanisa la Ufunuo Jimbo la Geita Heryyabwana Majebele alisema serikali imefanya jambo jema kujenga lami mji wa ushirombo hali ambayo ni kuweka muonekano mzuri wa mji na kuwapunguzia changamoto ya vumbi wafanyabiashara wa vibanda kado ya barabara za mitaa hadi sitendi ya mabasi.

Mkazi wa mji wa Ushirombo Magret Paul alisema iwapo serikali itakamilisha barabara ya lami itawasaidia kuondoa changamoto ya vumbi zinazo sababishwa na boda boda na magari ya abiria hasa wajasiliamali walio kando ya barabara hapa Ushirombo.

Afisa Tawala Wilaya ya Bukombe Ally Mketo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba alitoa wito kwa wananchi kutunza miundo mbinu ya miradi inayo endela kutekelezwa na serikali.
Wakati huo huo Mketo aliwaomba viongozi wa madhehebu ya dini kuhamasisha wananchi kuunda vikundi ili wanufaike na mkopo wa vijana, wanawake, na watu wenye ulemavu.

Comments