Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mkoa wa Geita, Said Nkumba amepiga
marufuku wanafunzi kuingia kwenye kumbi za starehe ili kulinda maadili wanapo
kuwa shuleni na kwenye jamii ikiwa shule ya sekondari Ushirombo ina wanafunzi 1658 kati yao 14 wamesimamishwa masomo
na uongozi wa shule hiyo kwa kosa la uvutaji wa madawa ya kulevya na kufanya
uhalifu wakuteka wenzao huku wengine wakifanya biashara ya ngono.
Nkumba alitoa agizo hilo kwenye kikao cha wazazi na walezi wa
shule ya sekondari Ushirombo baada ya Mwalimu wa nidhamu shule ya sekondari
Ushirombo Happyness Charles kusema Ofisi yake kwa kufuata sheria na mioungozo
ya shule wanafunzi 14 wamesimamishwa masomo kwa siku 21 tangu Agosti 11 na siku
zinaisha wakati huu walikizo fupi hadi Sepetmba 16 shule ikifunguliwa bodi
itakuwa imekaa na kuchukua maamzi stahiki kwa wanafunzi hawo.
Charles alisema kati ya wanafunzi waliosimamishwa 14 kati yao
wavulana 12 msichana 1 kwa makosa mbali
mbali likiwemo la kuvuta dawa za kulevya na msichana 1 amesimimishwa kwa
kufanya biashara ya kujiuza mwili wake.
“Agizo la serikali ya Wilaya litasaidia wanafunzi kutopata
vishawishi vya utumiaji madawa ya kulevya na mavazi yasiyo ya kimaadili kwa
wasichana na wavulana hasa nguo za kubana (modo) na kwamba wanafunzi wengi
wamekuwa wanaingia kwenye kumbi za starehe kwa ruhusa ya wazazi na walezi kwenda
kudansi shoo kwenye kumbi za harusi” alisema Charles
Kwa upande wake Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Bukombe Philibert
Nyangahondi aliwaomba wazazi na walezi kushirikiana na walimu kuwajengea uwezo
wa kiutamaduni wa maadili mema na kuhakikisha wanafuatilia maenedeleo ya
wanafunzi mashuleni.
Nkumba aliagiza bodi ya shule kukaa kikao na kuhakiki upya
majina ya wanafuzi septemba 10 ikiwa ni kabla ya likizo fupi kuisha na watakao
bainika wanahatia wafukuzwe shule.
Nkumba akitoa angizo kwa Mkuu wa Polisi Wilaya Elisha Kusula kuhakikisha
siku 30 anakamata wauzaji wa bangi, na wamiliki wa bar wanaotoa ajira kwa wanafunzi
na kufanya dolia ya mara kwa mara.
Nae Kusula alisema atatekeleza maagizo siku 30 ni nyingi
atakuwa amesafisha mji wa Ushirombo.
“situmi mtu”alisema
Mkuu wa Polisi Wilaya.
Miongoni mwa wazazi waliokuwa wamehudhuria kikao hicho Scholastika Zefania alisema chanzo cha wanafunzi kujiingiza kwenye
tabia ya uvutaji bangi na kujiuza chanzo ni wazazi hasa wa kiume wamekuwa
wakitelekeza familia na kuazisha nyumba ndogo na mzingo kubaki kwa akina mama.
Mohamed Hames alisema chanzo cha madili kuporomoka ni
wanawake wamekuwa wakivaa nguo zisizo na maadili na kusifiana mbele ya watoto
wao hali ambayo inawaadhirili watoto kujiingiza kwenye tabia mbovu shuleni na jamii
kwa ujumla.
Comments
Post a Comment