Timu ya Buselesele fc yatwa ubingwa
kwa kuibuka naushindi wa mabao 4-1 timu ya Kibehe fc mchuano wa fainali
mashindano ya Karemani cup 2019 katika uwanja wa Chato wilayani chato mkoa wa
Geita.
Mfungaji wa timu ya Buselesele fc
goli lakwanza Emmanuel Shimla dakika ya 39 huku goli tatu yakifungwa kwa
mikwaju ya penaliti baada ya dakika 90 kuisha timuzote zikiwa sale ya 1-1
mfugaji wa goli la Kibehe fc Ezekiel Kalisho dakika ya 78 huku timu hiyo katika
mikwaju ya penaliti haikufunga hata goli moja nakuipa Buselesele fc ubingwa.
Katibu mkuu chama cha mpira wa miguu
wilaya ya Chato (CDFA) Wilfred Machugu amesema kuwa mashindano hayo yalianza
Juni 20 na fainali imefanyika Septemba 15 mashindano hayo yalishirikisha timu
115 namichuano ilianzia ngazi ya vijiji kata tarafa hadi wilaya.
Machugu alisema lengo la ligi hiyo
nikuibuwa vipaji na kuhakikisha wanapata timu itakayo shiriki daraja la tatu
hadi la kwanza na kunawachezaji 10 wamesha chukuliwa na timu ambazo zinashiriki
ligi kuu Biashara Unaited, Kagera shuga.
Mshindi wa kwanza timu ya Buselesele fc ambao
nimabingwa walitwa kitita cha fedha sh 1 milioni na ng’ombe wawili jezi seti
mbili na mpira mmoja huku mshindi wa pili Kibehe fc wakibeba sh 700,000 na
mbuzi wa wili jezi seti moja mpila mmoja, mshindi wa tatu Nyuki fc alibeba sh
500,000 na jezi seti moja na mpira mmoja huku mshindi wa nne timu ya Selengeti
fc aliambulia sh 300,000 jezi seti moja na kuku wa wiili.
Akikabidhi dhawadi hizo mkuu wa mkoa
wa Geita Robart Gabriel aliwataka vijana kuendeleza vipaji vyao na sio
kujiingiza kwenye makundi mabaya ambayo yanaweza kuhatalisha maishayao na
kwamba michezo ni ajira na inajenga urafiki na afya pia.
Mzamini wa mashindano hayo mbuge
jimbo la chato ambae pia waziri wa nishati Dk Edward Kareman alisema kaulimbiu
ya mashindano hayo nikuhamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura kuchaguwa
kiongozi bora wakuwaletea maendeleo katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakao
fanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Fainali za mashindano hayo
yalihudhuliwa na mbunge wa jimbo Bukombe ambae pia waziri wa madini Doto Biteko
na mbunge wa jimbo l a Geita mjini ……Kanyasu na viongozi wengine mbali mbali
huku uwanja ukiwa umefulika mamia ya wananchi.
kama kawaida yetu mashabiki
Mchuano ikiendelea uwanjani
Mhe Medard Kalemani ambae ni mbunge wa jimbo la chato ambae pia ni mdhamini wa mashindano ya Kalemani cup 2019
Mkuu wa mkoa wa geita Mhe. Mhandisi Robert Luhumbi akikabidhi zawadi kwa washindi
Mkuu wa mkoa wa geita Mhe. Mhandisi Robert Luhumbi akizungumza jambo na wabunge waliohudhuria kwenye mashindano
Kama Kawaida yetu mashabiki
Mhe.Constantine Kanyasu ambae ni mbunge wa Geita Mjini akizungumza jambo baada ya kumalizika kwa mashindano
Mhe Doto Biteko katika juhudi za kuunga mkono katika fainali ya Kalemani cup
Mhe Doto Biteko katika juhudi za kuunga mkono katika fainali ya Kalemani cup
Mhe Doto Biteko katika juhudi za kuunga mkono katika fainali ya Kalemani cup
Comments
Post a Comment