Mbunge wa Jimbo la Bukombe
mkoani Geita, Doto Biteko amewataka wananchi wa Kata ya Namonge Wilaya ya
Bukombe kuwa mstari wa mbele kuchangia miradi ya maendeleo.
Biteko aliyasema hayo wakati akihutubia
wananchi wa kata ya Namonge kwenye mkutano wa hadhara akitoa mchango wa mifuko 200
ya saruji yenye thamani ya Tsh milioni 3.7 itakayo saidia ukamilishaji wa
ujenzi wa Kituo cha Afya na choo kwa ajili ya wagonjwa.
Biteko aliwataka viongozi wa kamati
ya maendeleo ya kata kusimamia kikamilifu ili mradi ukamilike mwaka huu na kuondoa
changamoto ya wakazi wa kata hiyo kutembea umbari mrefu wa kilomita 12 toka
Namonge hadi kata ya Uyovu kwa ajili ya kufuata huduma.
Wakati huo huo Mbunge Biteko ametoa mifuko
78 ya saruji yenye thamani ya sh 1.4 milioni na mabati 10 yenye thamani ya sh 200,000
shule ya msingi Namonge kwenye ujenzi wa Choo cha wanafunzi matundu 20.
Diwani wa Kata ya Namonge Mhe. Mulalu
Bundala alisema wananchi wamekuwa wakitembea umbari mrefu kutafuta huduma za
Afya na mradi ulianza 2013 malengo ya kukamilika ni mwaka 2019 mradi mpaka sasa
umegharimu sh 52 milioni huku nguvu za wananchi sh 8 milioni.
Mkuu wa shule ya msingi Namonge Jemes
Masumu alisema ujenzi wa choo hadi kukamilika utagharimu sh 11.3 milioni lakini
msada wa mbunge wa mifuko 78 ya saruji itakamilisha mradi huo na kwamba fedha
nyingine imetolewa na halmashauri na wadau wa maendeleo.
Masumu alisema choo cha wanafunzi
kilititia Mei 3 mwaka 2019 shule hiyo inawanafunzi 3315 wavulana 1644 wasichana
1671 wanajisaidia kwenye choo cha matundu sita ambacho hakikidhi mahitaji wengine
kulazimika kutumia choo cha muda kilichozungushiwa nyasi.
Comments
Post a Comment