WAZIRI BITEKO APIGA MARUFUKU SHUGHULI ZA UCHIMBAJI WA MADINI YA BAUXITE KATIKA MILIMA YA BUGHAI WILAYANI LUSHOTO
WAZIRI wa Madini Doto Biteko
akizungumza na wananchi wa Kata ya Magamba wilayani Lushoto mkoani Tanga
wakati wa ziara yake kutembelea eneo milima ya Bughai kulikokua
kunafanyika shughuli za uchimbaji wa madini ya Bauxite baadae kuzungumza
na wananchi kupitia mkutano wa hadhara.
WAZIRI wa Madini Doto Biteko
kushoto akisisitiza jambo kwa Diwani wa Kata ya Magamba Mathew Mbaruku
wakati wa ziara yake katikati anayeshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Lushoto
January Lugangika
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza kwenye mkutano huo
MBUNGE wa Jimbo la Mlalo Rashid Shangazi akizungumza wakati wa ziara hiyo ya Waziri wa Madini Doto Biteko
MKUU wa wilaya ya Lushoto January Lugangika akizungumza
DIWANI wa Kata ya Magamba (CCM)
Mathew Mbaruku akizungumza wakati wa mkutano huo kushoto ni Waziri wa
Madini Doto Biteko kulia ni Mbunge wa Jimbo la Mlalo (CCM) Rashid
Shangazi
WAZIRI wa Madini Doto Biteko akiingia kwenye eneo la Milima ya Bughai kulikokua kukifanyika uchimbaji wa madini ya Bauxite
Wananchi wa Kata ya Magamba wakimsikiliza Waziri wa Madini Doto Biteko
Wananchi wa Kata ya Magamba wakimsikiliza Waziri wa Madini Doto Biteko
Wananchi wa Kata ya Magamba wakimsikiliza Waziri wa Madini Doto Biteko
Waziri wa Madini Doto Biteko kulia akimsikiliza kwa umakini Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mazinde Juu wakati wa mkutano huo
Waziri wa Madini Doto Biteko
amepiga marufuku kuendelea kwa shughuli za uchimbaji wa madini ya
Bauxite katika milima ya Bughai mpaka hapo utafiti wa athari za
mazingira utakapofanyika.
Marufuku hiyo ameitoa kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Magamba wilayani Lushoto
wakati wa ziara ya kutembelea eneo hilo na baadae kuzungumza na wananchi
kupitia mkutano wa hadhara.
Amesema kuwa hakuna shughuli za uchimbaji zitakazofanyika mpaka
hapo watakapoweza kupata majibu sahihi ya athari za kimazingira katika
eneo hilo.
“Nimepiga mafuruku shughuli zote
za uchimbaji kuendelea kwani nimeona kuna mashine kule za uchimbaji
hivyo ziondoeni “amesema Waziri huyo.
“Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa wilaya
naomba mlisimamie hili Lakini wakati tunaendelea kufanya hilo zoezi wale
walikuwa na mashine pale lazima tujue ni wakina nani na wanapeleka wapi
hiyo Bauxite “Alisema
Waziri huyo pia amemtaka Afisa
Madini mkoa wa Tanga kufanya uchunguzi wa kiasi cha Madini
kilichochimbwa ili kuweza kuwachukulia hatua wahusika wote waliochimba
bila ya kufuata utaratibu kwa sababu hawajaruhusu uchimbaji kutoka
wakati huo.
Awali akizungumza katika mkutano
huo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella aliwataka wananchi kuwa
wasikivu na kama kuna mahala wanahitaji ufafanuzi watapatiwa ili kuondoa
sintofahamu kuhusiana uwepo wa madini hayo.
Alisema kwamba kumekuwa na haya madini watu wa madini watakuja
kutoa elimu hapa na waziri amekuja kuja kuona haya madini na kuona namna
ya kuyaendeleza.
Mkuu huyu wa mkoa alisema kama ipo
sheria inasema nini na kama kuna suala la kisheria kwenye suala la
uchimbaji lazima kuzingatiwe sheria na taratibu zilizopo kwa maslahi ya
Taifa.
Awali akizungumza wakati wa ziara
ya Waziri huyo Afisa madini Mkazi wa Mkoa wa Tanga Zabibu Napacho
alimueleza Waziri huyo kwamba kwenye maeneo waliopewa ruhusu ya
uchimbaji kuna mgogoro ulioanza muda mrefu tokea mwaka 2001 mpaka sasa.
Alisema kwamba hilo linatokana na
wananchi kuwa na uelewa tofauti kuhusiana na uchimbaji wa Bauxite kwa
ujumla kutokana na kuona kama utaondoa uoto wa asili na kuchafua
mazingira kwa hiyo wananchi hawajaukubali mradi huo
Afisa Madini huyo Mkazi alisema pamoja na kwamba wadau wenye
leseni za uchumbaji walichukua juhudi za kufanya utafiti za kuangalia
athari za mazingira lakini lengo lao halikutimia kwa sababu wakati
wakiendelea na mchakato huo ukaingiliwa.
Hata hivyo alisema inaonekana
halmashauri na serikali wanaukubali huo mradi lakini wachache hawana
uelewa kuhusu mradi huo kikubwa wananchi wanapaswa kupewa elimu
kuhusiana na uchimbaji huo.
Comments
Post a Comment