Mashindano ya ligi ya Doto Cup 2019
yakiendelea kutimua vumbi katika michezo ya Fainali kusaka ubingwa wa tarafa
ambapo timu ya Runzewe Academy ya kata ya Uyovu imetwaa ubingwa wa tarafa ya
siloka kwa kuilaza mabao 6-0 timu ya Namsega kutoka kata ya Runzewe mashariki.
Mchuano huo wa fainali ulifanyika uwanja
wa michezo kata ya Uyovu almarufu uwanja wa mwenge.
Wafungaji wa magoli ya Runzewe
Academy Felix Malango alifunga magoli matano dakika ya 1 na dakika ya 27,
dakika ya 49 na dakika ya 50 pia dakika ya 69
goli la sita lilifungwa na Magazi Doto dakika ya 86.
Kocha wa timu ya Runzewe Academy
Hobbu Mangire alisema ushindi huo wamepata kwa mpango wa mungu tangu kikosi chake
kianze mashindano ya ligi ya Doto Cup 2019 hakijafanya vibaya kwa mashabiki
wake na imewahi kuchukuwa makombe ya Doto Cup mwaka 2016 na 2017 wamekosa kombe hilo mwaka 2018 kwani
lilichukuliwa na Bukombe Star huku akiwahakikishia mashabiki wake kuwa mwaka
huu pia ni zamu ya Runzewe Academy.
Kwa mjibu wa katibu mkuu wa chama cha
mpira wa miguu wilaya ya Bukombe (BUFA) Bosco Mwidadi amesema katika mchezo
uliokuwa unatimu vumbi uwanja wa Bugelega kutafuta bingwa wa Tarafa ya Bukombe
kati ya timu ya Bukombe star na timu ya Chui fc.
Amesema timu ya Chui fc ya Bugelenga
imeibuka na ubigwa wa Tarafa ya Bukombe baada ya kuichapa bao 1-0 timu ya Bukombe
star mfugaji wa timu ya Chui fc Musa Jemes dakika ya 61 hadi kipenga cha mwisho timu ya
Bukombe star walikuwa hawaja funga.
Comments
Post a Comment