Timu ya runzewe academy fc ya kata ya
Uyovu imeilisha bao 2-0 timu ya Nampagwe fc ambayo ilikuwa bingwa wa kata ya
Runzewe magaribi katika mchuwano uliofanyika katika uwanja wa Uyovu kutafuta timu
itakayo ingia fainali kusaka bingwa wa tarafa ya Siloka mashindano ya ligi ya
Doto Cup 2019.
Wafungaji wa magoli ya timu ya
Runzewe adademy Mathayo Jeremia dakika ya 20 na goli la pili lilifungwa na
Magazi Doto dakika ya 64 hadi kipenga cha mwisho cha mwamzi Nampagwe fc
hawakufunga na kuwafanya kutoka kwenye mashindano hayo.
Katibu mkuu wa chama cha mpira wa
minguu wilaya ya Bukombe (BUFA) Bosco Mwidadi amesema katika mashindano ambayo yalikuwa bado yanaendelea huku tarafa zingine
zime maliza muzunguko mapema wiki hii.
Mwidadi alisema fainali ya kusaka
bingwa tarafa ya siloka itachezwa katika uwanja huo Agost 7 na timu ya Namsega
fc na Runzewe Academy sikuhiyo itaenda
sambaba na kukutanisha na timu za Chuif
na Bukombe Star kutafuta bingwa
wa tarafa ya Bukombe mchuwano huo utafanyika uwanja wa Bukombe.
Agost 5 mwaka huu katika viwanja
viwili tofauti tarafa ya Ushirombo na tarafa ya kimichezo Bulega zitakutanisha
timu nne kusaka bingwa kila tarafa ambapo timu ya Nsagali fc ambaye
nibigwa wakata ya Ng’anzo itakutana na Sinamila fc bingwa wa kata ya Butinzya katika
uwanja wa Bulega timu ya Ushirombo Worrios bigwa wa kata ya Bulangwa itachuwana
na timu ya Kilimahewa fc bigwa wa kata ya Katente katika uwanja wa Ushirombo
mjini.
Comments
Post a Comment